26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mbunge Haonga aachiwa kwa dhamana

Na Arodia Peter, Dodoma

Mbunge wa Mbozi mkoani Songwe, Pascal Haonga ambaye alikamatwa jana na Jeshi la Polisi mkoani humo ameachiwa kwa dhamana.

Wakili wa mbunge huyo, Gaston Gatubindi ameliambia MTANZANIA Digital leo Mei 7 kuwa Haonga ameachiwa kwa dhamana na anatakiwa kuripoti kwa mpelelezi wa Mkoa wa Dodoma keshokutwa.

Wakili amesema kabla ya kupewa dhamana polisi walikwenda nyumbani kwa mbunge huyo kufanya upekuzi kwa mujibu wa taratibu.

Aidha baada ya kupewa dhamana, Haonga alikwenda moja kwa moja bungeni kuendelea na kikao cha bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Baada ya kuingia bungeni Haonga alishangiliwa kwa nguvu na wabunge karibu wote wa upande wa upinzani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles