25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mbunge Chadema akamatwa na polisi Dodoma

Mwandishi Wetu, Dodoma

Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga (Chadema), amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma leo Jumatatu Mei 6, wakati akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyoendelea.

Mtanzania limefika Kituo cha Polisi Mkoa wa Dodoma kushuhudia mbunge huyo akihojiwa kwenye Ofisi ya Upelelezi ya Mkoa wa Dodoma.

Hata hivyo haikujulikana mara moja sababu za kukamatwa mbunge huyo.

Alipotafutwa kwa simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto simu yake iliita bila kupokewa.

Akizungumzia tukio hilo, Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema hawajapata taarifa rasmi kwanini mbunge huyo amekamatwa.

“Huu ni mwendelezo wa matukio ya viongozi wetu kukamatwa, licha kwamba walitakiwa kujulisha uongozi wa bunge,” amesema Silinde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles