23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kagame, Sall kuunguruma mkutano wa wajasiriamali wa Tony Elumelu

Abuja, Nigeria

Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Rais wa Senegal, Macky Sall, wanatarajiwa kuwa wazungumzaji wakuu katika warsha itakayoambatana na mkutano wa tano wa wajasiriamali  ulioandaliwa na Taasisi ya Tony Elumelu Foundation (TEF).

Mkutano huo utakaofanyika nchini Nigeria Julai 26-27, mwaka huu ambapo pamoja na marais hao, mwasisi wa TEF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Heirs Holdings na Benki ya United Bank for Africa (UBA), Tony Elumelu, watakuwa katika majadiliano ya wazi.

Mkutano huo wa kila mwaka  huandaliwa kupitia Programu ya ‘Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship’ ambayo imewapa mafunzo Waafrika chipukizi 3,000 ambao walichaguliwa kutoka zaidi ya waombaji 216,000. 

Tukio hilo linawapa nafasi wanawake na wanaume chipukizi kutoka nchi 54 za Afrika kukutana, kujifunza na kubadilishana mawazo yenye mlengo wa kuwa wawekezaji bora Afrika na duniani.

Pia ni fursa muhimu kwa viongozi wanasiasa na watunga sera kukutana na kizazi kipya cha wafanyabiashara viongozi Wafrika ambao wanabadilisha uchumi wa Afrika.

Uwepo wa marais hao unawapa fursa wajasiriamali kutoka Afrika wanaohudhuria kuwa na mjadala wa kina na kutoa ushuhuda namna serikali inavyoweza kufanya kuchochea ukuwaji wa biashara.

Ajenda ya mkutano huo inahusisha majadiliano na wataalamu kutoka Afrika na duniani ambao watawapa mafunzo washiriki kuongeza ujuzi katika biashara yao.

Aidha warsha hiyo itawapa fursa baadhi wajasiriamali wateuli kuelezea bidhaa na huduma wanazotoa mbele ya jopo la majaji.

Mikutano hiyo imewahi kuhudhuriwa  na marais kadhaa wakiwamo Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, Waziri Mkuu wa mstaafu wa Benin na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri, Lionel Zinsou na Makamu wa Rais wa Nigeria, Profesa Yemi Osinbajo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles