Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mbunge wa Viti Maalum, Agnesta Kaiza (Chadema) amehoji
kuhusu madai ya wastaafu watalipwa lini fedha zao bunge Mbunge huyo Kijana alihoji deni hilo la wastaafu juzi Jijini hapa alipokuwa akichangia hotuba ya Rais Dk. John Magufuli ya kuzindua Bunge la 12 .
Kaiza amesema kuwa kitendo cha Serikali kudaiwa na mifuko ya Jamii ndio kimesababisha wastaafu kutopatiwa mafao yao kwa wakati hivyo suala hilo linaitia doa serikali.
“Kitendo cha serikali kudaiwa na mifuko ya Jamii, ndio imesababisha wastaafua wetu kutopatiwa mafao yao kwa wakati, hivyo serikali ina mpango gani kulipa madeni hayo”, alihoji Kaiza.
Hata hivyo mbunge huyo wa Chadema licha ya kuhoji suala hilo alisifia kazi nzuri inayofanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama.
Aidha, Mbunge huyo amesema kutolipwa kwa wastaafu hao kumepelekea wawe katika maisha magumu baada ya kustaafu.
Aidha, amehoji kuhusu madeni wanayodai baadhi ya wakandarasi waliokuwa wakifanya shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini.
“Sio wastaafua tu hata makandarasi nao wanaidai Serikali madeni ya muda mrefu, Serikali nayo iangalie jinsi ya kuwalipa ili hawa watu wapate haki yao”, alisema Mbunge huyo.
Akijibu swali hilo, Waziri Mhagama amesema serikali imeshalipa trillioni 2 waliokuwa wakidaiwa na mfuko wa Pensheni wa watumishi wa Umma (PSSSF).
Aidha Mhagama alisema Serikali inaendelea kuhakiki madeni yote inayodaiwa kwa lengo ya kuyalipa.
Wabunge wa Chadema au wa Chachandu?