26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Kiaani afurahia ‘Distance Love’ kuingia Afrika Mashariki

Accra, Ghana

Msanii wa miondoko ya Afrobeat na Dancehall kutoka Ghana, Stephen Kofi Annan maarufu kama Kiaani, amewashukuru mashabiki wa Afrika Mashariki kwa mapokezi ya wimbo, Distance Love aliouachia hivi karibuni.

Kiaani ambaye ameanza muziki Novemba, 2017 kwa kuachia ngoma yake, Ame Bye Wo iliyotengenezwa na Garzy chini ya lebo ya Triff Music, ameshangaa kuona Distance Love inaingia kwenye chati mbalimbali za muziki Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki tofauti na matarajio yake.

“Huu ndio muda wa kueendelea kuwapa raha mashabiki zangu wa East Africa kwa upendo waliouonyesha kwenye wimbo wangu Distance Love ambao tayari unapatikana kwenye mitandao yote ya kusikiliza na kununua muziki duniani pamoja na chaneli yangu ya YouTube, nashukuru uongozi wangu wa Triff Music kwa kufanikisha hili,” amesema Kiaani.

Mwimbaji huyo mwenye vipaji vingi alizaliwa huko Prampram, Accra, Ghana, Desemba, 28, 1991 na akasoma shule ya msingi Nkwantanang kabla hajajiunga na sekondari ya Hillview ambapo alianza kuonyesha sanaa na baadaye akakutana na lebo ya Triff Music inayosimamia muziki wake kwa mafanikio makubwa mpaka sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles