25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CRDB kuibua vipaji vya vijana kuelekea tamasha Sauti za Busara

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Benki ya CRDB imeendeleza jitihada zake za kuwawezesha vijana kupitia vipaji kwa kuandaa shindano la muziki kuelekea tamasha la Sauti za Busara msimu wa 18 linalotarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar Februari 12 hadi 13, mwaka huu.

Akizungumza jana Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif, amesema dhamira ya benki ni kutoa fursa ya kimaisha na ajira kwa vijana na kuongeza ushiriki wao katika sanaa ya muziki.

“Muziki unapendwa na watu wengi na umetoa fursa nyingi kwa vijana ndiyo maana Benki ya CRDB imedhamiria kuwawezesha vijana kwa kuandaa shindano la kutambua vipaji vyao hasa kwenye muziki,” amesema Farid huku akibainisha kuwa uwezeshaji huo ni mwendelezo wa jitahada za muda mrefu zinazofanya za kuwasaidia vijana wajasiriamali katika sekta mbalimbali za maendeleo kupitia mafunzo, mikopo na utafutaji wa masoko.

Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif, akizungumza wakati wa kutangaza udhamini wa benki hiyo katika tamasha la Sauti za Busara sambamba na kuibua vipaji vya vijana.

Amesema waliendesha shindano la kutambua vipaji vya vijana kupitia mitandao yao ya kijamii ambapo vijana walikuwa wakijirekodi wakiimba kisha kusambaza katika akaunti zao za mitandao ya kijamii na zile zilizopendwa zaidi (likes) na kupewa maoni na watu wengi ziliingia hatua ya pili ya kupigiwa kura.

Amesema aliyepata kura nyingi ndiye aliibuka mshindi ambapo atapelekwa katika tamasha hilo na kugharamiwa usafiri, chakula, malazi na kupata fursa ya kuunganishwa na huduma mbalimbali za benki hiyo.

Benki hiyo pia imetangaza kudhamini tamasha hilo kwa Sh milioni 25 ili kuendelea kuunga mkono ajenda ya kukuza utalii ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Farid amesema kupitia tamasha hilo pia wanahamasisha wananchi kutumia njia mbadala za kibenki kama Simbanking, CRDB Wakala, Internet Banking na nyingine na kuchana kutembea na fedha taslimu.

“Njia mbadala za kibenki ni rahisi na salama na zinapunguza ulazima wa kutembea na fedha taslimu. Katika msimu huu pia kutakuwa na punguzo la bei kwa baadhi ya migahawa hapa Zanzibar tukihamasisha watu kutumia kadi zao kufanya malipo na hata kununua tiketi kupitia tembocard au CRDB Wakala,” amesema.

Naye mshindi wa shindano la kuibua vipaji Richard Mucho maarufu kama @mucho_flows ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuendesha shindano hilo na kudhamini tamasha hilo na kwamba hatua hiyo itaongeza mapenzi ya muziki kwa vijana kama ilivyo kwa burudani nyingine.

“Nimefurahi kuibuka mshindi katika shindano la kuibua vipaji ambavyo kwa sehemu kubwa ni ajira kwa vijana, naishukuru Benki ya CRDB kwa kubuni kitu hiki naamini jitihada hizi zitawahamasisha vijana wengi kushiriki,” amesema Mucho.

Benki ya CRDB kupitia sera yake ya Uwezeshaji katika Jamii (CSI) imekuwa ikiwekeza kwa vijana ili kuongeza ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.

Mwaka jana benki hiyo pia iliendesha mashindabo ya CRDB Bank Taifa Cup ambayo yalifanyika katika viwanja vya Chinangali Dodoma ambapo vijana 26 walipata udhamini wa benki hiyo kwenda kusoma katika vyuo mbalimbali nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles