26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mbunge Chadema adai Serikali kusema ‘sheria ya vicoba’ inabana utakatishaji fedha ni uongo

Mwandishi Wetu, Dodoma



Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema), amepinga hoja ya Serikali kuwa moja ya sababu za kutungwa kwa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, ni kukabiliana na utakatishaji wa fedha haramu.

Peneza amesema hayo leo Alhamisi Novemba 15, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia muswada huo ambao umewasilishwa Bungeni kwa hati ya dharura na unatarajiwa kupitishwa kesho.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati akisoma muswada huo kwa mara ya pili, amesema moja ya sababu ya kutungwa kwa sheria hiyo ni kuwepo kwa mianya ya uatakatishaji fedha haramu kutokana na taasisi za huduma ndogo ya fedha kutokuwa na uratibu wa kisheria unaozitaka kutekeleza matakwa ya Sheria ya Udhibiti wa Utakatisha Fedha haramu.

Akichangia muswada huo, Peneza amesema watu ambao wanaguswa sekta hiyo wengi ni wanawake ambao wanachangishana Sh 500 ama 1,000 kwa wiki ama mwezi.

“Hapa suala la kutakatisha fedha hakuna, ni bora tuangalie namna ya kusaidia hawa watu ambao wengi wao hata kusoma hawajui, sasa ukiwaletea mambo ya kwenda kujisajili wengi watashindwa,” amesema.

Pia ametaka suala la faini liangaliwe kwa sababu Bunge likitunga sheria na kanuni kwenda kutungwa kwingine kunaweza kuwa chombo hicho kinatumika kuumiza wananchi bila kujua.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles