31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

DSTV ‘kukiwasha na familia’ msimu wa sikukuu

Johns Njozi, Dar es Salaam



Kampuni ya Multichoice Tanzania imezindua huduma mpya kuelekea msimu wa sikukuu yenye kauli mbiu ‘Ni muda mzuri wa kukiwasha na familia’ kupitia king’amuzi chake cha DSTV.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Novemba 15, wakati wa uzinduzi Meneja Masoko wa Multchoice, Alpha Mrio, amesema wateja wa DSTV sasa watapata burudani zaidi za kusisimua kama vile Soka, Filamu, Tamthilia, Katuni na vipindi mbali mbali vya watoto vitakavyoileta familia pamoja katika msimu huu wa sikukuu na kudumisha upendo.

“Mwaka huu kama kawaida umekuwa mwaka wa neema kwa wateja kwani tumekuwa na mfululizo wa zawadi kwa wateja wetu,” amesema Mrio.

Akifafanua kuhusu ofa hiyo, Mkuu wa Mauzo wa Kampuni hiyo, Salum Salum, amesema hiyo ni zawadi ya kufunga mwaka kwa wateja wapya wa DSTV kwani katika kipindi cha miezi miwili wataweza kuunganishwa na DSTV kwa gharama ya Sh 79,000 tu na kupewa kifurushi cha bomba mwezi mmoja bure.

“Mbali ya kuongezwa kwa chaneli na maudhui kwenye DSTV, pia kwa wale ambao hawajajiunga hatujawasahau sasa tunawapa ofa kabambe ya kujiunga kwa gharama nafuu na wapate kifurushi cha bomba mwezi mmoja bure,” amesema Salum.

Amesema ofa hiyo itadumu kwa muda wa miezi miwili nchi nzima kuanza Novemba 15.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles