31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge ampongeza Rais Samia

Na Ramadhan Hassani, Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuupa kipaumbele Mkoa wa Dodoma katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwamo sekta ya maji, elimu na miundombinu, huku akiwaomba wananchi wa Kata ya Handali kumchagua mgombea udiwani wa kata hiyo, Emmanuel Madali.

Mariam ametoa kauli hiyo, wakati akimnadi mgombea huyo  kuelekea uchaguzi mdogo baada aliyekuwepo kujiuzulu nafasi hiyo katika mkutano wa hadhara na wananchi hao.

Amesema Rais Samia ameyagusa maisha ya wananchi wa Dodoma ambapo katika sekta ya elimu ametoa kiasi cha bilioni 12 ambapo jumla ya madarasa 601 yatajengwa bila wananchi kuchangishwa.

“Dodoma tuna bahati kubwa, Rais wetu Samia Suluhu Hassan ametupatia fedha shilingi  bilioni 12.02 ambazo zimeelekezwa katika kutatua changamoto ya Madarasa mkoani kwetu ambapo madarasa 601 yatajengwa, lakini pia ametupatia bilioni 3.5 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa shikizi 175, hii haijawahi kutokea.

“Kama hiyo haitoshi hapa Wilaya yetu ya Chamwino ambayo sisi Kata ya Handali tupo, Rais Samia ametupatia jumla ya bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 64 lakini pia ameleta fedha kwa ajili ya shule shikizi 14, haya yote Rais Samia amefanya kwa mapenzi yake makubwa kwetu sisi wananchi wake,” amesema.

Amesema katika sekta ya nishati Rais Samia ameonesha kiu yake ya kumaliza changamoto ya umeme kwa wananchi ambapo katika kata hiyo tayari vitongoji 15 kati ya 21 vimeshafikiwa na hivyo vilivyobaki ndani ya mwaka wa fedha wa 2021/22 vitakamilishwa.

“Rais wetu anataka kuona Mkoa wetu wa Dodoma unapaa kimaendeleo, tayari ameidhinisha kiasi cha bilioni 127 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato ambapo pia Benki ya Maendeleo ya Afrika imetoa Dola Milioni 327 kukamilisha uwanja huo utakaokua ukihudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka. “Kwa hiyo ndugu zangu wa Handali naombeni mumchague diwani Emmanuel Madali ili aweze kushirikiana na Mbunge wetu Lusinde na Rais Samia kusukuma maendeleo ya kata yetu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles