Ramadhan Hassan
Mbunge wa Viti Maalum, Mariamu Kisangi (CCM) amehoji Serikali ina mpango gani wa kupeleka mashine za kufulia nguo katika Hospitali za Dar es salaam.
Akiuliza swali bungeni leo Jumanne Mei 21, Kisangi amesema kwamba Hospitali za Dar es salaam hazina mashine za kufulia nguo, Je ni lini Serikali itatoa mashine hizo.
Akijibu swali hilo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Serikali imejipanga kutoa huduma zote za afya ikiwemo kununua mashine za kufulia katika Jijini la Dar es salaam.
“Tumejipanga kuboresha huduma zote na kununua mashine na madaktari bingwa naomba nilichukue tutatoa majibu ni lini ila tumeanza kuagiza,” amesema Ummy.