31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE ABOOD AWAPA SOMO WANAHABARI

abood

Na Ramadhan Libenanga

-MOROGORO

MBUNGE wa Morogoro Mjini, Aziz Abood (CCM), amewataka wanahabari mkoani hapa wahakikishe wanaisoma kwa makini Sheria ya Huduma kwa vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ili waweze kuandika habari zenye masilahi kwa umma na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro (MOROPC).

“Timizeni wajibu wenu kwa mujibu wa taaluma yenu ili  kuiletea sifa taaluma ya habari nchini,” alisema.

Pamoja na raia hiyo, Abood aliwataka wanahabari kujiwekea malengo ya kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya kisera.

Mbunge huyo aliunga mkono kazi zinazofanywa na wanahabari, huku akipinga hatua ya baadhi ya mitandao ya kijamii kushusha heshima za watu, kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha usalama wa nchi na watu wake.

“Wanahabari kalamu zenu kama mtazitumia vizuri, ni wazi mtakuwa mmeisaidia Serikali ya Rais Magufuli ambayo imekuwa ikihangaika kujenga uchumi na maendeleo kwa watu wote,” alisema Abood.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles