NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM |
LICHA ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutoa dhamana kwa viongozi sita wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, hatua hiyo haijaweza kuwafanya wanasiasa hao kusherehekea Pasaka wakiwa uraiani.
Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama hiyo kuamuru viongozi hao wafikishwe mahakamani Aprili 3 kutimiza masharti ya dhamana zao baada ya jana kudaiwa kushindwa kufikishwa kutokana na gari kuwa bovu.
Hali hiyo imejitokeza jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati mahakama ilipokaa kutoa uamuzi wa kuwapa ama kuwanyima washtakiwa dhamana.
Mahakama iliamua kutoa uamuzi wa kuwapa dhamana washtakiwa bila wenyewe kuwapo kwa masharti kwamba wawe na wadhamini wawili kila mmoja, wenye barua na vitambulisho, wasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 20 na washtakiwa wanatakiwa kuripoti polisi kila Alhamisi.
HALI ILIVYOKUWA MAHAKAMANI
Awali Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, alidai washtakiwa hawapo mahakamani na katika kufuatilia kwa uongozi wa Magereza Segerea walipo na kwa Inspekta Shabani, taarifa iliyopatikana ni kwamba mahabusu wote kutoka gereza hilo hawakufika mahakamani.
Akitoa maelezo, Inspekta Shabani, alidai alipata taarifa kwa msaidizi wa Mkuu wa Gereza la Segerea, kwamba gari lililowabeba washtakiwa lilipotoka gerezani liliharibika, hivyo kwa siku ya jana hakuna mahabusu kutoka Segerea ambao wangefika mahakamani.
“Gari mpaka muda huu halijatengemaa, uwezekano wa kuwaleta mahabusu umeshindikana,” alidai Inspekta Shabani.
Hakimu Mashauri alisema kutokana na hoja hizo, mahakama itatoa …
Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.