32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mbowe kuongoza mazishi ya Mtoi

MBOWENa Waandishi Wetu, Dar na Tanga

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe leo anatarajiwa kuongoza wananchi wa mkuza wakati wa mazishi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa chama hicho Jimbo la Lushoto mkoani Tanga, Mohamed Mtoi Shemng’ombe (39).

Mtoi alifariki dunia juzi jioni, baada ya gari lake alililokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka kisha kuingia kwenye korongo wilayani Lushoto.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Habari  na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene alisema chama chake kimepokea kwa masikitiko kifo hicho.

Alisema tayari vikao vya chama, vimeshaitishwa kwa ajili ya kupanga tararibu za mazishi.

“Mazishi yatafanyika kesho (leo) saa 7:00 mchana Mkuzi  nyumbani kwa marehemu, Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe ataongoza mazishi hayo,” alisema Makene.

Alisema marehemu Mtoi ameacha mke mmoja na watoto wawili.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji  aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana, kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi saa 2;30 usiku katika Kijiji cha Magamba Coast.

Alisema  gari hilo aina ya Land Rover Discover, lililokuwa likiendeshwa na  Miraji Nuru (43) mkazi wa Mkuzi wilayani humo, lilikuwa likitokea tarafa ya Mlola kwenda Mkuzi baada ya kumaliza shughuli zao za kampeni.

“Ukiangalia mazingira ya ajali hii, utaona dereva alikuwa mwendokasi, pale alipopatia ajali kulikuwa na kona kali iliyomshinda kukata na kujikuta akingia kwenye korongo,”alisema Kamanda Mwombeji.

Alisema ajali hiyo, ilisababisha abiria wote waliokuwamo kupata majereha na kukimbiwa Hospitali ya Wilaya Lushoto kwa matibabu.

Alisema wakati wakiendelea na matibabu, Mtoi alifariki dunia kutokana na majeraha aliyopata eneo la ajali.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Lushoto, Dickson Shekivuli alisema  baada ya kumaliza mkutano wa kampeni walirudi ofisini kwa ajili ya vikao vya tathimini na kumaliza saa mbili usiku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles