30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Dylan Kerr aishika pabaya African Sports

kerr kazini simba 34NA ONESMO KAPINGA, TANGA

KOCHA Mkuu wa Simba Mwingereza, Dylan Kerr, ni kama aliwashika pabaya wachezaji wa African Sports baada ya kufanya uamuzi wa kwenda kuwasoma kabla ya kuvaana kwenye mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo amekiri alikuwa sahihi kwani aliweza kutambua uwezo wa mshambuliaji wao hatari, Novat Lufungo.

Kabla ya kukutana na African Sports juzi kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Kerr alishawasoma wapinzani wake na kugundua umahiri wa mshambuliaji huyo hatari ambaye alilazimika kumpa majukumu beki, Jjuuko Murushid ili aweze kumkabili.

Baada ya kugundua Lufungo anaweza kuwaliza na kuwanyima ushindi wa kwanza Ligi Kuu, Kerr aliyeshuhudia mechi ya kirafiki kati ya Coastal Union na African Sports alimpa Murshid jukumu la kumkaba baada ya kutambua usumbufu wake anapokuwa uwanjani.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kerr alisema baada ya kuisoma African Sports kwa dakika tisini walipocheza na Coastal Union, alibaini Lufungo ni mshambuliaji hatari ndani ya kikosi hicho hivyo kulazimika kumuandalia ulinzi wa kutosha.

“Safari yangu ya kuja mkoani Tanga kwa ajili ya kuishuhudia African Sports ilinisaidia sana kujua uwezo wa wachezaji wa timu hiyo ndiyo maana nimeweza kupanga kikosi imara ambacho kimeweza kuwakabili vilivyo,” alisema.

Licha ya kuibuka na ushindi, kocha huyo aliyeiongoza Simba katika mechi ya kwanza Ligi Kuu juzi, aliisifia African Sports kwa kucheza soka lenye ushindani huku akieleza kuwa haikuwa kazi rahisi kupata matokeo hayo kutokana na ugumu waliopata kutoka kwa wenyeji wao.

Kerr alisema amefurahishwa na matokeo ya ushindi ugenini kwani malengo yake ni kuhakikisha wanapata pointi zote sita katika michezo miwili watakayocheza kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Simba ambao wameondoa mkosi wa kutoshinda kwenye Uwanja wa Mkwakwani, keshokutwa wanatarajia kushuka tena dimbani kucheza na wababe wao Mgambo Shooting ambao mara ya mwisho waliwafunga mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu mzunguko wa pili msimu uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles