25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mbinu za asili za kupunguza uzito

matunda

NA DK. JOACHIM MABULA,

KABLA ya kukimbilia kujinyima vyakula ili kupunguza uzito, inabidi uamue ni uzito gani unaouhitaji. Wataalamu hawashauri kushusha uzito ghafla kwa zaidi ya paundi 50 ndani ya wiki moja.

  1. Tambua mahitaji ya kalori (nguvu)
    Kabla hujaamua jinsi ya kula, unapaswa kufahamu ni kalori (nguvu) kiasi gani unahitaji kwa siku. Hii inaweza kupatikana kwa kikokotozi maalumu cha kalori (nguvu) kinachotumia kimo, uzito, umri na shughuli za mhusika.
  2. Jifunze kutumia matunda na mboga za majani
    Unahitaji walau vipande vitano vya matunda na mboga za majani. Kufanya
    hivi kutaweka mwili wako vizuri kwa kuwa matunda na mboga za majani vina nyuzi muhimu (valuable fibres) na vitamini muhimu. Pia vinajaza tumbo lako na hufanya usihitaji kula vyakula vya kalori (nguvu) sana.
  3. Angalia kiwango cha chakula unachotumia
    Jizuie kula vyakula vyenye nguvu sana mfano maharagwe ya soya, mafuta ya samaki, soseji, karanga n.k na ukilazimika kula kwa kiwango kidogo. Dondoo ya muhimu ni kutafuna chakula chako taratibu na kwa muda unaofaa ili kurahisisha umeng’enyaji wa chakula na hii itakusaidia kula kidogo.
  4. Usiruke mlo
    Wengi wanaotaka kupunguza uzito huona kujinyima milo mfano kuacha kula mchana au asubuhi au usiku ndio njia sahihi wakati si sahihi, kula chakula kidogo kutafanya mwili uwe na afya. Unaweza hata kugawa ile milo mitatu mikubwa katika vijisehemu vitano au sita vya muda mfupi.
  5. Matunda na mboga safi ya asili ndio sahihi zaidi
    Vyakula vilivyosindikwa viwandani vina sodiamu na mafuta kwa wingi. Unatarajiwa kushusha uzito ukitumia vyakula asili.
  6. Usidhibiti matumizi ya vyakula
    Unaweza kuendelea kula vyakula unavyopenda kama vipande vya keki
    lakini hakikisha unatumia kwa tahadhari kubwa vitu hivyo vyenye sukari ili visiwe vipingamizi vya kushusha uzito wako.
  7. Usiamini kila kitu kilichoandikwa kwenye lebo za vyakula
    Lebo zinazosema haina mafuta haimaanishi kuwa kuna kiwango kidogo cha kalori(nguvu). Ni sawa na zile lebo zinazosema kiwango kidogo cha sukari (low sugar).
  8. Dhibiti kiwango cha vinywaji vya sukari unavyokunywa.
    Unywaji wa soda na juisi za viwandani huongeza utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kufanya uzito kuongezeka. Jitahidi kunywa glasi nane za maji safi na salama ambayo yatasaidia kutoa sumu na uchafu mwilini.
  9. Ainisha vyakula utakavyokula
    Kuandika mpangilio wa vyakula utakavyokula kutakulinda na kuhakikisha vyakula vya kutia nguvu unavyokula ni sahihi, pia ni kikumbusho cha kila wakati juu ya ni vyakula gani unahitaji.
  10. Kumbuka kufanya mazoezi kila siku
    Dakika 30-60 za mazoezi kila siku zitalinda afya yako na kukusaidia
    kupunguza uzito. Mazoezi ya kunyanyua vitu vyenye uzito ni mazuri zaidi kwa kuwa huchoma kalori iliyopo mwilini.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles