24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mbinu mpya ya kudhibiti mbu waenezao malaria

Jamii Yetu Pull Out. Siah.inddMALARIA ni ugonjwa wa kuambukiza u n a o l e t w a na chembe chembe zinazojulikana kwa jina la kitaalamu plasmodium.
Chembe chembe hizi huingia ndani ya mwili wa binadamu baada ya kuumwa na mbu jike aina ya Anopheles.
Mbu mwenye chembe chembe za plasmodium anapomuuma mtu, humuingizia baadhi ya mate yenye viini vya
kuambukiza kwenye kidonda, hivyo kusambaza malaria.

Viini hivi husafiri hadi katika maini ambapo hukaa hadi vifikie ukomavu.
Kuna aina 4 za malaria, ambazo ni P. vivax, P. malariae, P. ovale na P. falciparum. Zimepewa majina kulingana
na aina ya plasmodium inayozisababisha. Aina 3 za kwanza si hatari lakini falciparumni ni hatari mno na hata inaweza kusababisha kifo kwa haraka zaidi.

Hii ni kwa sababu ikishaingia tu mwilini huzaana kwa wingi ndani ya damu. Chembe chembe nyekundu za damu (ambazo husambaza oksijeni mwilini), zilizoathirika huwa nzito na haziwezi kuingia kwenye kapilari. Hali hii
husababisha kufa kwa sehemu ya ubongo, maini, mapafu, figo na matumbo kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni, jambo ambalo husababisha kifo kama haita tibiwa haraka.

Dalili za malaria ni pamoja na homa, kutetemeka, maumivu ya viungo, kutapika, anemia (inayosababishwa na
kuachana kwa chembechembe nyekundu za damu), kuumwa kichwa na kuharibika kwa retina. Dalili hizi hujitokeza
kila baada ya siku mbili kwa maambukizi ya P. vivax na P. ovale, wakati dalili za P. malariae na P. falciparum hujitokeza kila baada ya siku tatu.

Inaweza kuambatana na homa inayojitokeza kila baada ya kati ya saa 36-48 au homa isiyoshadidi lakini inayoendelea.
Watoto walio na malaria mara nyingi hudhihirisha mkao usiokuwa wa kawaida, ishara ya uharibifu wa ubongo. Imegunduliwa kuwa malaria husababisha matatizo ya kutambua hasa kwa watoto.
Pia husababisha kuenea kwa anemia katika kipindi cha kukua haraka kwa ubongo na uharibufu wa moja kwa moja
wa ubongo.
Uharibifu huu wa kinurolojia hutokana na malaria ya ubongo ambayo ni hatari mno kwa watoto. Malaria ya aina hii uhusishwa na uweupe wa retina, ambayo inaweza kuwa na manufaa kama ishara ya kutofautisha malaria na visababishi vingine vya homa.

Shirika la Afya Duniani (WHO) liliwahi kutoa ripoti kwamba katika kipindi cha mwaka 2013, zaidi ya watu milioni 198 waliambukizwa malaria na imekadiriwa kuwa watu 584,000 walikufa kutokana na ugonjwa huo.
Karibu watu wanne kati ya watano waliokufa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Karibu nchi 100
duniani huathiriwa na ugonjwa huu hivyo kutishia maisha ya watu wengi.

Inakadiriwa kuwa watu bilioni 3.2 duniani wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa malaria.
Ili kukabiliana na ugonjwa huo, wataalamu wa kisayansi wamebaini njia mpya ya kutia dawa za kuua mbu kwenye vyandarua.

Njia hiyo imefanikiwa kwa asilimia 100 katika kukabili baadhi ya aina za mbu. Ripoti ya utafiti wa kimataifa inasema njia hiyo inayotumia nguvu za umeme za elektrostatiki kupaka dawa huwezesha vyandarua kubeba viwango vya juu vya dawa.
Wakati wa kufanyiwa majaribio, dawa iliyotiwa kwenye vyandarua kwa njia hiyo, ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama electrostatic coating, iliua mbu wengi kuliko kawaida.

Wakiandika katika jarida la afya la Proceedings of the National Academy of Sciences, watafiti kutoka Uholanzi wanasema njia hiyo inaweza kusaidia kukabiliana baadhi ya magonjwa kama vile malaria ambao unatishia maisha ya watu wengi duniani.

“Mbu kuzoea dawa limekuwa tatizo sugu katika maeneo mengi yanayotatizwa na malaria duniani.
“Inadhaniwa kuwa dawa za maji za kunyunyizwa pamoja na neti za vitanda, ambazo wakati mwingine huwa na
viwango vya chini vya dawa, huwa mara nyingi haziui mbu hivyo kuwafanya kuzoea dawa,” ulisema utafiti huo.

Katika utafiti wa sasa, watafiti kutoka Uholanzi walitumia sehemu yenye nguvu Mbinu mpya ya kudhibiti mbu waenezao malaria za umeme, iliyotayarishwa awali kwa kunasa chavua hewani na kuipaka dawa.

Kutumiwa kwa nguvu za umeme aina ya electrostatic zinazodumu muda mrefu, kuliwezesha viwango vya juu vya dawa kujishikilia upesi na vema katika vyandarua, hivyo kuhakikisha mbu wanapata dawa ya kutosha kuwaua
mara tu wanapogusa neti – hata kama ni sekunde chache. Mbinu hiyo ilifanyiwa majaribio kwenye aina tofauti
za mbu nchini Afrika Kusini, Tanzania na kwenye maabara ya kitivo cha dawa za maeneo yenye mvua nyingi cha
Liverpool.

Watafiti walibaini kuweka dawa kwa kutumia nguvu hizo za umeme kuliwezesha kuuawa kwa mbu wengi, ikilinganishwa na neti zilizopakwa dawa kwa njia nyingine na kwa baadhi ya mbu ambao wamekuwa hawasikii dawa, ilifanikiwa kwa asilimia 100.

Utafiti huo ulisema; “Neti za kawaida huua chini ya asilimia 10 ya mbu.”
Aliyeongoza utafiti huo, kutoka In2Care – Chuo Kikuu cha Wageningen nchini Uholanzi, anasema njia hiyo ya kupaka dawa inaweza kutumiwa katika vitambaa vya kufunika madirisha, milango, kwenye mitego ya mbu na
mashimo ya kupitishia hewa majumbani.

“Ni njia mpya ya kulenga kuwafikia na kuwapa dawa mbu,” anasema.
Aidha, anasema njia hiyo mpya itafaa kwa kuwa inaweza kutumiwa na aina mbalimbali za dawa.
Hata hivyo, anasema njia hiyo ya kupaka dawa huenda haifai kwa neti za kufunika vitanda kwa sababu watu huzigusa mara kwa mara na kwa hivyo dawa hiyo inaweza kutoka baada ya muda.

Makala haya yameandaliwa kwa msaada wa Shirika la Habari la BBC. 0715789922.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles