25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mbelgiji Simba afichua siri ya kung’ang’aniwa Dar

NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

BAADA ya kulazimishwa suluhu na Lipuli FC, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema rekodi za msimu uliopita michezo kati  ya timu hizo ndio zilizochangia kikosi chake kukosa pointi tatu.

Simba ililazimishwa suluhu na Lipuli katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yalikuwa mwendelezo kwa kikosi cha Simba kushindwa kuvuna pointia tatu tangu Lipuli iliporejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, baada ya kushuka daraja.

Timu hizo zilitoka sare katika michezo miwili ya msimu uliopita, ikianza sare ya bao 1-1 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kabla ya sare ya idadi hiyo hiyo Uwanja wa Samora, Iringa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Aussems, alisema anaamini rekodi za msimu uliopita kati ya timu hizo ziliwafanya wachezaji wake kupoteza hali ya kujiamini na kusababisha wapoteze umakini.

“Tulijiandaa vizuri, lakini Lipuli ilikuwa bora zaidi, niliangalia rekodi zao dhidi yetu msimu uliopita na kubaini, hatukuweza kupata pointi tatu, hali hii ilinifanya nitabiri mchezo mgumu.

“Tulijitahidi kupambana kushinda ili kujiweka vizuri kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mbabane Swallows, lakini tulikutana na timu inayotufahamu, nafurahi kupata mechi za aina hii, kwani zinazidi kutujenga, tumepoteza nafasi nyingi za kufunga, mambo kama hayo ni kawaida kwenye mpira, tumekubaliana na matokeo, tunakwenda kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo,” alisema Aussems.

Wakati Aussems akifichua kilichomponza, Kocha Mkuu wa Lipuli, Suleiman Matola, alisema walifanikiwa kuvuna pointi moja Dar es Salaam, baada ya kuziba mianya ya wapinzani wao aliodai wana utamaduni wa kujaza viungo wengi ili kutawala mchezo.

“Tunajua Simba ni timu nzuri, sisi tulifanya utafiti wetu na kubaini silaha yao kubwa ni viungo wengi, ili tuweze kupambana nao vizuri, lazima tujaze viungo katikati ya uwanja, nashukuru mpango huo ulifanikiwa,” alisema Matola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles