29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Phiri apewa jukumu Mbabane Swallows kuimaliza Simba

NA MWANDISHI WETU

ZIKIWA zimesalia siku chache kabla ya kuikabili Simba katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uongozi wa Klabu ya Mbabane Swallows ya Swaziland umefanya marekebisho katika benchi lao la ufundi na  kumkabidhi Kinnar  Phiri  kuwa kocha mkuu wa timu yao.

Phiri ambaye ni raia wa Malawi, aliwahi kuinoa Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya kuamua kuachana nayo.

“Tumempa kazi ya muda mfupi Kinnah ili aongoze timu yetu katika michuano ya kimataifa kwasababu kocha wetu anatumikia adhabu,” alisema Meneja wa Mbabane Swallows, Sandile Zwane.

Alisema Thabo Vilakati  anatumikia adhabu ya kusimamishwa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia mwokota mipira wakati wa mchezo.

Mabadiliko hayo yamekuja siku chake ikiwa kikosi hicho kinajiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo itavaana na Simba Jumatano iyajo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Zwane alisema wanaamini Phiri atawasaidia kuwapa mbinu za kuikabili Simba, kwakuwa anaifahamu kwa undani timu hiyo baada ya kufundisha Ligi Kuu Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,400FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles