23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa kukutwa na misokoto 400 ya bangi

Safina Sarwatt, Moshi

Jeshi la polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia, Stephano Anthon(30) mkazi wa Kibosho Moshi kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina bangi misokoto 400.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 4, 2021 Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amesema Anthony alikamatwa Desemba 29, 2020 saa 9:50 alasiri katika kata ya Mawenzi.

Kaimu Kamanda amesema kuwa mtuhumiwa huyo Anthon alikutwa na bangi misikoto 400 ambapo inadaiwa kutwa kwenye mfuko zikiwa zimeviringishwa kwenye shuka la kimasai.

Makona amesema kuwa mtuhumiwa huyo ni msafiridhaji na ni muuzaji wa bangi, na kwamba anashikiliwa na jeshi hilo na atafikishwa mahakamani.

Wakati huohuo jeshi hilo linawashikiliwa watu wa tano kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya magari(Muffler compound powder) kifaa kinachosaidia kuipa gari nguvu.

Kaimu Kamanda amewataja watuhumiwa hao kuwa, Peter Mtui (44) mfanyabiashara na mkazi wa Rombo ambaye alilinunua kifaa hicho kwa, Athuman Muro (36) fundi magari stend ya Mboya.

Wengine ni mkazi wa shirimatunda, Rashindi Mkwizu (24) Ramadhani Kitokota (30) na Hamadi Mwarabu (32)

“Katika kipindi cha mwisho mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka 2021 jeshi la polisi limefanya misako mbalimbali mkoani humu kwa lengo la kuhakikisha usalama dhidi ya uhalifu na kwamba misako hiyo imefanikisha kuwakamata watuhumiwa hao wa wizi wa vifaa vya magari.

Kaimu Kamanda huyo amesema watuhumiwa wote wanahusika na matukio ya wizi wa kifaa hicho kwa kushirikiana na waosha magari na mafundi magari ambao sio waminifu na kwamba upelelezi unaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles