27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa kubaka mtoto wa miaka mitatu

GUSTAPHU HAULE -PWANI

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Dismas Slyvester (35), mkazi wa Mlandizi wilayani Kibaha, akituhumiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 19, mwaka huu saa 9 alasiri, Kata ya Mlandizi.

Alisema inadaiwa mtuhumiwa ambaye ni fundi ujenzi, alimuiba mtoto huyo na kutokomea naye vichakani, kisha kufanya ukatili huo.

Kamanda Nyigesa alisema baada ya taarifa kufikia jeshi hilo kupitia raia wema, walianza kushirikiana na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na mtoto katika shamba la mbogamboga ambalo liko vichakani.

“Jeshi la Polisi linawashukuru raia wema waliotoa taarifa hizi, maana lilichukua hatua mara moja na kuanza msako, hatimaye kumkamata mtuhumiwa  vichakani akiwa na mtoto,” alisema Kamanda Nyigesa.

Alisema uchunguzi unaonyesha mtoto huyo ameingiliwa kimwili na sasa taratibu zinaendelea kufanyika ili sheria ichukue mkondo wake.

Katika tukio jingine, Mariam Shomari (25), mkazi wa Msongola Mlandizi, ameibiwa mtoto wake mchanga Swaum Sudi mwenye umri wa miezi mitatu akiwa ndani amelala.

Kamanda Nyigesa alisema mtoto huyo aliibwa Agosti 25, saa moja jioni na mtu asiyejulikana.

Alisema Mariam aliondoka kwenda nyumba ya jirani umbali wa mita 200 kuomba kibiriti, huku akimwacha mtoto mchanga ndani akiwa na dada yake, Fatima Sudi.

Kamanda Nyigesa alisema mbinu aliyotumia mwizi huyo, ni kuvizia na kuingia ndani na kumweleza Fatima kuwa ametumwa na mama yake kumchukua mtoto ili ampelekee, kitendo kilichofanya afanikiwe.

Alisema polisi wanaendelea na msako, huku akiwaomba viongozi wa Serikali wakiwamo watendaji wa kata, wenyeviti wa vitongoji na raia wema kutoa taarifa pale ambapo watagundua mtu mwenye mtoto aliye na shaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles