26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

MBARAWA ASHAURI BENKI ZITOE  MIKOPO YA  RIBA NAFUU

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amezialika benki nchini kushiriki katika kutoa mikopo ya riba nafuu katika miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano ikiwamo katika sekta za miundombinu.

Profesa Mbarawa alisema hayo     alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 100 ya   Benki ya Standard Chartered   Dar es Salaam juzi usiku.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi wa juu wa benki hiyo kutoka sehemu mbalimbali duniani   na wateja wakiwamo wafanyabiashara wakubwa nchini.

Alisema Serikali ya   Rais John Magufuli, pamoja na mambo mengine, imechukua hatua kadhaa  kuhakikisha Taifa linapiga hatua katika uchumi ikiwamo kuimarisha miundombinu, kupambana na rushwa na kuongeza ufanisi katika serikali.

Alisema Tanzania ni nchi ya 11 ambayo uchumi wake unakua kwa kasi kwa mujibu kwa takwimu za 2015 (unakua kwa asilimia saba) na kwa Afrika, ni ya sita kwa nchi ambazo uchumi wake wa viwanda unakua kwa kasi.

“Nafahamu kwamba Benki ya Standard Chartered ina uzoefu mkubwa wa kuunga mkono miradi ya miundombinu katika Afrika na sehemu nyingine duniani.

“Kwa hiyo wakati mnapoadhimisha miaka 100 ya shughuli zenu nchini   itakuwa jambo jema kama mtafanya tathmini ya fursa za kuwekeza katika miradi ya miundombinu ya usafiri na sekta nyingine ambazo ni kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Tano,” alieleza.

Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, ujenzi wa barabara tano za juu katika makutano ya baadhi ya barabara   Dar es Salaam, ujenzi wa viwanja vya ndege, bandari na vyombo vya usafiri wa majini.

“Kwa hiyo  ninaziomba benki nchini kuja kuzungumza na serikali na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kusaidia miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Tano.

“Tunaikaribisha Standard Chartered na benki nyingine kutumia fursa hii ya serikali kujitokeza kufadhili miradi hiyo, lakini tunasisitiza kuwa lazima waje na mikopo yenye riba nafuu   Watanzania wasibebeshwe mzigo mkubwa wa kulipa fedha hizo,” alisema.

 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani aliahidi kuwa benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao.

Alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali katika kukuza uchumi wa nchi kwa kutoa huduma bora na stahiki kwa wananchi na kuchangia kutimiza dhana ya Tanzania ya Viwanda kufikia mwaka 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles