27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mbarawa aagiza wananchi kuunganishiwa maji kwa mkopo

Na Sam Bahari, Shinyanga

WAZIRI wa Maji Profesa, Makame Mbarawa, amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi  na Usafi wa Mazingira Kahama (Kuwasa), Allen  Marwa, kuwaunganishia ya wananchi maji kwa makubaliano ya kufanya malipo kwa awamu.

Profesa  Mbarawa alisema hayo alipokuwa kwenye ziara ya siku mbili kukagua miradi ya maji mkoani Shinyanga jana.

 “Pamoja na kazi nzuri mnayoifanya ya kulaza Mabomba kutawanya huduma ya maji kwa wananchi, mnapaswa kujua kuwa wateja wenu ni pamoja na hawa watu hivyo wakopesheni hiyo huduma ya maji walipe kidogokidogo” alisema Mbarawa.

Mbarawa alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (Shuwasa) Flaviana Kifizi kwa kandarasi ya ujenzi wa tenki lililojengwa katika Kata ya Busoka, Kahama kwa kutumia watalamu wa Shuwasa.

Tenki la Kata ya Busoke lenye ujazo wa lita za ujazo milion 600 limegharimu Sh bilion 2.5 kutoka mapato ya ndani ikilinganishwa na makadirio ya awali ya Sh bilioni 4.6 iwapo kama wangetumika wakandarasi wa nje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles