26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

‘Maziwa ya awali ya mama ndio msingi wa mtoto kupata virutubisho muhimu’

Na Hadija Omary Lindi

Maziwa ya awali ya mama ndio msingi wa mtoto kupata virutubisho muhimu vitakavyoweza kumfanya awe na kinga za kutosha katika kupambana na magonjwa katika ukuwaji wake.Hayo yameelezwa na Afisa Lishe wa Manispaa ya Lindi mkoani humo, Mwenda Gela alipokuwa anazungumza na Mtanzania Digital ofisini kwake hivi karibuni

Mwenda amesema kuwa zipo baadhi ya Imani walizonazo akina mama hasa wa vijijini wakiamini kuwa maziwa ya mama ya mwanzo ni machafu kulingana na rangi yake hivyo hayafai kwa motto aliezaliwa kwani yanaweza kumletea madhara.

Amesema maziwa hayo ya awali yajulikanayo kwa jina la kitaalamu (Colostrum) anatakiwa kupatiwa mtoto ndani ya saa moja hadi mbili baada ya kuzaliwa kwani maziwa hayo ya awali ni muhimu kwa mtoto kwa kuwa ubeba vitu vitatu muhimu ikiwa pamoja na potassium, protine , fat, vitamin A, B, E, na C ambavyo kwa kiasi kikubwa humsaidia mtoto kuwa na kinga mzuri katika kupambana na magonjwa.

Hata hivyo, mwenda ameeleza kuwa maziwa hayo ni rahisi kwa mtoto kumeng’enywa kwa kuwa yana kingamwili nyingi , chembechembe nyeupe za damu , yana viini vinavyomkinga mtoto na maradhi na vya ukuaji ambavyo husaidia utumbo wa mtoto mchanga kukua baada ya kuzaliwa.

Pamoja na umuhimu wa maziwa hayo ya mwazo ya mama pia Mwenda amesema ni muhimu pia kunyoyesha mtoto maziwa pekee kwa kipindi cha miezi sita bila kumpa chakula chochote kwani maziwa ndio chakula pekee cha mtoto kilicho salama.

Kwa kawaida maziwa ya mama hutengenezwa kipindi cha ujauzito, anapojifungua huanza kutoka kidogo na kuongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda na mtoto anavyonyonya yakiwa na virutubisho hivyo vya sukari ya lactose, protini, mafuta, vitamini na madini huku maji yakiwa ni sehemu kubwa yananayokidhi kiu ya mtoto kwa miezi sita ya mwanzo.

Naye Mtaalamu wa Afya ya Uzazi, Grecy Mrope kutoka katika Kituo cha Afya cha mjinii hapo amesema kuwa Licha ya wataalamu wa afya kusisitiza umuhimu wa kunyonyesha mtoto miezi sita ya mwanzo, bado kuna wanawake huogopa kunyonyesha wakihofia kupoteza mvuto wa maumbo yao.

“Wanawake wengi hasa wa mjini wanaamini kunyonyesha kuna haribu maumbile yao ikiwamo matiti kulala na miili yao kuwa mikubwa (kunenepa) kupitiliza, ambapo baadhi yao upelekea wanapojifungua huacha kunyonyesha watoto wao kwa makusudi wakiogopa kunenepa na matiti yao kulala,” amesema.

Naye, Mariam Juma Mkazi wa Manispaa ya Lindi amesema ni vizuri elimu ya faida ya maziwa ya mama kwa mtoto izidi kutolewa katika vituo vya kutolewa huduma za mama na mtoto mara kwa mara ili mama anayejifungua ajue hatari wanayoweza kuisababisha kwa watoto endapo wataacha kuwanyonyesha maziwa yao kwa makusudi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles