24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TFF mpya kujulikana kesho

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unatarajia kufanyika kesho, jijini Tanga ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba amesema ikifika saa 9: 00 Alasiri, viongozi waliopita watakuwa wamejulikana.

Akizungumzia maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi leo, Kibamba amesema Agenda Kuu itakuwa ni uchaguzi na asilimia 90 ya wajumbe wamesawasili Tanga kutokana maeneo mbalimbali.

“Kwa kifupi maandalizi yote yamekamilika, uchaguzi utafanyika kesho tarehe 7, Agosti, niwaombe Watanzania kuwa watulivu kwani itakapofika saa tisa , watakuwa wamejua ni viongozi  gani wamepata nafasi ya kuongoza mpira wetu kwa miaka minne,” amesema Kibamba.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa nafasi ya Urais, Wallace Karia hana mpinzani, huku mpambano ukiwa kwenye kinyang’anyiro cha Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao kila Kanda wapo zaidi ya mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles