24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maximo amkingia kifua Jaja

Marcio Maximo
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo, amemkingia kifua mchezaji wake, Mbrazil Genilson Santos ‘Jaja’ kwa kuwataka mashabiki wasitegemee vitu vingi kutoka kwa wachezaji warefu kwani wana vitu vichache vyenye mafanikio.

Maximo aliyasema hayo juzi baada ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya Thika United ya nchini Kenya iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Jaja, huku baadhi ya mashabiki wakihoji uwezo wake kutokana na kutoonyesha makeke zaidi uwanjani.

Alisema siku zote wachezaji warefu hawana vitu vingi lakini wana nafasi kubwa hasa wanapokuwa katika eneo la umaliziaji, kwani pale ndio wanaonekana umuhimu wao.

“Wachezaji kama Bonifance Ambani na John Bocco, ni wachezaji warefu lakini wana vitu vichache sana vizuri na ndio maana wanazidi kuonekana bora, hivyo wachezaji warefu hawana mambo mengi lakini kwa sasa sitaki kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja nataka kuizungumzia timu nzima kwa uwezo waliouonyesha uwanjani,” alisema.

Alisema, wachezaji wake wameanza kumuelewa na wameonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo kwani wameweza kubadilisha mchezo, mfumo na wameanza kuelewa licha ya makosa machache yaliyojitokeza ambayo atatumia wiki moja kuyarekebisha kabla ya kukutana na Azam FC katika mechi yao ya Ngao ya Hisani, Septemba 14, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Alisema, Thika ni timu nzuri na ni timu ngumu na yenye kasi lakini wachezaji wake wameweza kuikabili vema na hatimaye kuibuka mabingwa, hayo ni mafanikio makubwa kwake na anaimani kadiri siku zinavyokwenda timu yake itazidi kuwa timu bora zaidi.

Alisema, uwezo huo wa wachezaji wake unamuhakikishia kuwa wataibuka na ubingwa mbele ya Azam ambayo nayo ni timu nzuri yenye uwezo mkubwa, lakini watahakikisha wananyakuwa ubingwa mbele yao na kuanza vema Ligi Kuu msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles