25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Bocco, Moris watemwa safari ya Burundi

Timu ya Taifa, Taifa Stars
Timu ya Taifa, Taifa Stars

NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kimeondoka leo alfajiri kuelekea mjini Bujumbura, kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyo katika Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Burundi, huku wachezaji sita wakitemwa katika safari hiyo.

Wachezaji hao waliotemwa katika msafara huo kwa ajili ya mechi itakayochezwa Jumapili mjini humo, ni John  Bocco, Aggrey Morris, Mwagane Yeya, Edward Christopher, Said Juma na Said Ndemla.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Stars, Boniface Clemence, alisema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mart Nooij, amewaacha wachezaji hao kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo viwango vyao na wengine kuwa  majeruhi.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Stars, Mart Nooij, alisema mchezo huo utakuwa muhimu kwani iwapo watashinda Tanzania inaweza kupanda katika viwango vya FIFA.

“Nimeupa umuhimu mkubwa mchezo wa Jumapili kutokana na kuwepo kwenye kalenda ya ubora wa viwango vya FIFA, hivyo tunahitaji ushindi wa aina yoyote ili tuweze kuwapo katika nafasi nzuri,” alisema Nooij.

Aliwataja wachezaji walioondoka katika msafara huo unaondoka kwa Shirika la Ndege la Kenya, kuwa ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Mwadini Ali, Oscar Joshua, Shomari Kapombe, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Joram Mgeveke, Erasto Nyoni, Himid Mao, Salum Abubakar na Haruna Chanongo.

Wengine ni Khamis Mcha, Simon Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto, Said Morad, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa na Juma Liuzio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles