24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

MAWAZIRI WAELEZA KUZOROTA KWA TAZAMA

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

HATUA ya kusuasua kwa utendaji wa Kituo cha Kusafisha Mafuta cha Indeni Petroleum Refinery Limited cha Ndola, nchini Zambia ni sababu mojawapo iliyochangia kuzorota kwa ufanisi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta la Tazama.

Hayo yemeelezwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na Zambia mara baada ya kukamilisha ziara ya siku nne ya kutembelea mkuza wa Bomba la Kusafirisha Mafuta ghafi la Tazama na vituo vya kusukuma mafuta na kuzungumza na wafanyakazi wa vituo hivyo.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kwamba kiwango cha bomba kimeshuka ikilinganishwa na hapo hapo awali kwani lilikuwa na  uwezo wa kusafirisha lita za ujazo tani milioni 1.1 za mafuta kwa mwaka lakini kwa sasa linasafirisha lita za ujazo tani 600,000 tu.

Usafishaji wa mafuta unaofanywa na kituo hicho cha Indeni hauendani na usafirishaji wa bomba la Tazama na hivyo kuwa ni miongoni mwa sababu zinazochangia Bomba hilo kutofikia malengo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles