24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakili wanolewa kupambana na uhalifu mtandaoni

Na Ashura Kazinja, Morogoro

Mawakili wa Serikali nchini wametakiwa kutekeleza majukumu yao kuendana na mabadiliko mbalimbali yakiwemo ya sheria na taratibu, ili kuweza kukabiliana na uhalifu wa makosa ya mtandaoni.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya makosa ya mtandao kwa Mawakili wa serikali yaliyofanyika mkoani Morogoro, ambapo aliwaasa mawakili hao kufanya kazi kwa kufuata sheria na mabadiliko ya teknolojia ili kuweza kukabiliana vyema na vitendo vya uhalifu.

Amesema ni muhimu mawakili wa serikali kupatiwa mafunzo mbalimbali juu ya sheria na mabadiliko ya teknolojia kwani wakati mwinginne wahalifu wanatumia udhaifu au mianya iliyopo wazi kutenda uhalifu.

“Wengi tumeshuhudia makosa ya jinai kwa njia ya mtandao kama wizi, kusambaza picha na taarifa za uongo, na vitisho kwa njia ya mtandao vikizidi kushamiri kutokana na kukua kwa tenolojia,’’ amesema Simbachawene.

Akizitaja baadhi ya changamoto zinazopelekea makosa ya kimtandao kuzidi kuongezeka alisema ni uelewa mdogo wa baadhi ya watendaji wa Taasisi muhimu za kiuchunguzi na uendeshaji hasa katika eneo la makosa ya kimtandao.

Aidha aliwataka Mawakili hao kuhakikisha wanatenda haki katika majukumu yao kila siku kwani wao ni wawakilishi wa Mungu, na kwamba kutotenda haki na kutetea mkosaji kutawakosesha furaha na amani ya roho.

‘Kazi mnnayoifanya ni kazi yya Mungu, hivyo muwe na hofu ya Mungu msimamie haki, Mungu ndio anatoa haki, wewe unaesimamia haki ni mwakilishi wa Mungu, hivyo usiposimamia vyema haki unakuwa unakiuka kazi ya Mungu, mahakama hairilai kwenye teknikali zaidi, bali kuhakikisha haki inatendeka,” amesema.

Hata hivyo Waziri Simbachawene amewaahidi mawakili hao kuwa atasimamia upatikanaji wa nafasi za kwenda kusoma nje sambamba na kusimamia maslahi yao.

Nae Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Makosa ya kimtandao Monica Mbogo amesema lengo la semina hiyo ni kupeana uzoefu kuhusiana na makosa ya kimtandao, ambayo utendaji kazi wake unatokana na ukuaji wa teknolojia ya Tehamma.

“Makosa ya kimtandao sio mapya, ni makosa yaleyale ya zamani,lakini yamekuwa advanced kwa kutumia teknnolojia ambayo inatutaka na sisi tubadilike kwa maana ukusanyaji wa ushhahidi na uendeshaji wake mahakamani unatofautiana kidogo na yale ya zamani,’’ amesema Mbogo.

Mmoja wa Washhiriki wa mafunzo hayo Wakili wa Serikali ofisi ya Taifa ya Mashitaka mkoa wa Singida, Apolinary Bagenda alisema makosa ya mtandaoni yanaongezeka kila siku, hivyo kama hawatapata mafunzo ya kuwajengea uwezo mara kwa mara watabaki nyuma na wahalifu kuwa mbele.

“Makosa ya kimtandaoni ni makosa yanayoibuka kila kukicha, wahalifu wa mtandaoni wako macho hawalali, hivyo tusipopata mafunzo tunaweza kuwa nyuma, hauwezi kupambana na mtu aliyekuzidi uwezo,”amesema Bagenda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles