23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Dk. Gwajima awataka MEWATA kulinda afya za akina mama

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Doroth Gwajima amekitaka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kuendeleza jitihada za kulinda afya za akina mama kutokana na mchango wao katika uzalishaji, malezi, makuzi na kuimarisha uchumi wa kaya.

Kauli hiyo ameitoa leo Februari 25,2022 jijini hapa wakati akifungua mkutano Mkuu wa 19 wa Chama cha Madaktari wanawake Tanzania (MEWATA).

Dk. Gwajima ameipongeza MEWATA kwa juhudi zao za kuleta maendeleo ya afya bora, hasa katika kupambana na magonjwa ya saratani yanayoshambulia wanawake kwa asilimia kubwa ikiwemo saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti.

Dk. Gwajima ameipongeza MEWATA  kwa juhudi zao za kuleta maendeleo ya afya bora, hasa katika kupambana na magonjwa ya saratani yanayoshambulia wanawake kwa asilimia kubwa ikiwemo saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti.

“Wito wangu kwenu, tuendeleze jitihada za kulinda afya za akina mama kwani wao ndio chimbuko la familia na nguzo muhimu ya maendeleo ya Taifa kutokana na mchango wao katika uzalishaji, malezi, makuzi na kuimarisha uchumi wa kaya,”amesema Dk. Gwajima.

Katika hatua nyingine, Dk. Gwajima amesema kutokana na umuhimu wa Chama hicho amewaomba kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na ugonjwa wa UVIKO-19 pamoja na umuhimu wa kuchanja kwani siku zote wao wapo karibu na jamii.

“Kwa mantiki hiyo, ushirikiano wa wataalamu wa sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii hususan wataalamu wanawake kuwa mstari wa mbele itaongeza tija zaidi.

“Mathalani MEWATA yenye wataalamu wanawake ikishirikiana na wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalamu itaweza kufikisha ujumbe wake kwenye jamii kwa ufanisi zaidi na siyo tu kwa UVIKO-19 bali hata kwa mambo mengine yanayohusu changamoto za afya.

“Kwa umoja huu wa MEWATA na Wataalamu wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii itawezekana kuhamasisha na kuelimisha jamii yakiwemo makundi maalum ili kuwandaa wananchi kupokea na kukubaliana na mabadiliko ya hali yoyote ya afya yanayojitokeza katika jamii,”amesema Dk. Gwajima.

Kwa upande wake Rais wa MEWATA, Dk.Mary Charles, ameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kuendelea kushirikiana na chama hicho katika mambo mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles