28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakili waja na hoja tatu kuiokoa ndege Afrika Kusini

Mwandishi Wetu

JOPO la Wanasheria kutoka Tanzania wameanza kupinga  uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Afrika Kusini wa kuizuia ndege ya Shirika la Ndege la ATCL.

Jopo la Mawakili hao wakiongozwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Ally Possi limeiambia Mahakama ya Gauteng kwamba yalifanyika makosa katika utoaji wa amri ya  kuikamata ndege hiyo.

“Tumeonyesha kuwa amri ya kuikamata ndege ya Tanzaniza aina ya airbus A220-300 ilitolewa kinyume dhidi ya serikali ya Tanzania na kwamba inapaswa kuondolewa,” wakili Tembeka Ngcukaitobi wa Afrika Kusini aliiambia mahakama.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu ya Gauteng, zinaeleza kuwa  serikali ya Tanzania pia imewasilisha hoja tatu nzito za kisheria kupinga uamuzi wa awali uliotolea na mahakama hiyo.

Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania, Wakili Damas Ndumbaro ambaye pia ni Naibu waziri wa Mambo ya Nje alikaliliwa na chombo kimoja cha habari sio MTANZANIA Jumamosi akisema kuwa anaamini mahakama imeelewa kasoro za uamuzi wa awali kupitia hoja hizo tatu ilizowasilisha na kwamba itatenda haki.

Wakili Mkuu Msaidizi wa Serikali Dk Ally Possi (katikati) akiwa na jopo lake la mawakili katika kesi ya kupinga kushikiliwa kwa ndege ya Airbus ya Tanzania wakati wa shauri hilo katika Mahakama Kuu ya nchini Afrika Kusini jana.

Ingawa hakufafanua hoja hizo anasema anaamini zitawarejeshea Watanzania haki yao ya kuipata ndege hiyo.

Ndumbaro ameahidi kueleza kwa kina msingi wa sheria wa hoja hizo tatu ambazo zimewasilishwa na mahakamani leo atakapozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Awali kabla ya kutua Mahakamani jana Naibu Wakili Mkuu wa serikali, Dk. Possi alikaririwa na gazeti la serikali la Daily News akisema kuwa timu ya wanasheria nane kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wenzao wa Afrika Kusini watafika mahakamani kupinga uamuzi huo

Kwa upande mwingine Wakili Roger Wakefied  ambaye katika kesi hiyo anamtetea Hermanus Steyn amesisitiza kuwa  kulikuwa kuna madai ya msingi katika shauri hilo.

Ndege hiyo ilizuiwa Agosti 23 kutokana na amri ya Mahakama Kuu ya Afrika Kusini ya Gauteng baada ya mapambano ya muda mrefu kati ya serikali ya Tanzania na mkulima mstaafu mzungu, Hermanus Steyn.

Steyn anadai kuwa mali zake Mali ikiwamo kampuni yake ya Rift Valley Seed Limited, shamba alilokuwa akimiliki binafsi ikiwamo vifaa, magari 250 na ndege ndogo 12 zilitaifishwa kinyume Januari 1982.

Inaelezwa kuwa alidai fidia ya Shilingi milioni 373 ambayo serikali ya Tanzania inaona si ya kweli.

Hata hivyo Jaji  Josephat Mackanja wa Mahakama Kuu ambaye kwa sasa amestaafu Julai 9, 2010 aliamuru Steyn alipwe Dola za Marekani 36,375,672.81.

Gazeti moja la Kiingereza  limendika kuwa upo ushahidi kwamba baada ya kutolewa kwa tuzo ya usuluhishi kulikuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili na kusababisha hati ya kutatuliwa kwa dola milioni 30 na baadaye serikali ya Tanzania ililipa sehemu kubwa ya kiasi hicho ili kumaliza madai hayo.

ILIVYOKAMATWA

Mwanasheria anayemwakilisha mlalamikaji Roger Wakefield wa kampuni ya mawakili ya Werksmans alisema kukamatwa kwa ndege hiyo kunatokana na amri iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Johannesburg Jumatano iliyopita.

Mteja wake ambaye amejitambulisha kama raia wa Tanzania mwenye asili ya Namibia iliamriwa na mahakama alipwe Dola za Marekani milioni 33 kama fidia iliyotokana na uamuzi wa kutaifisha mali zake, lakini serikali ilimlipa Dola milioni 20 tu.

Mwanasheria huyo anadai kuwa raia huyo wa Tanzania mwenye asili ya Namibia madai yake hayo yanatokana na serikali ya Tanzania kutaifisha shamba lake miongo kadhaa iliyopita.

Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya airbus yenye thamani ya Dola milioni 90  ilikamatwa Ijumaa iliyopita katika Uwanja wa ndege wa OR Tambo uliopo Johannesburg baada ya kutua kutoka Dar es Salaam.
 

kulingana na wakili ambaye hushauri migogoro ya mipaka kiasi cha dola milioni 16 kilichobaki ambacho Steyn anadai kilizaa riba ambayo sasa imefikia Dola za Marekani milioni 33.

Inaelezwa kuwa kwa miaka yote hiyo mkulima huyo alikuwa akipambana kupata kiasi hicho.

Inaelezwa kuwa wakati mali za mkulima huyo zikitaifishwa wakati huo alitangazwa kama mhamiaji haramu nchini Tanzania.
Hata hivyo wakili wake anasema madai hayo hayana msingi wowote, na sasa anaishi katika nchi nyingine ya Afrika Mashariki

Inaelezwa kuwa mkulima huyo aliwaendea wanasheria wa Afrika kusini, chini ya mkataba wa kimataifa wa kutekeleza usuluhishi wa migogoro ya kimataifa, kama njia ya kupata anayodai kwamba ilibaki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles