32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakili wa Serikali wapinga uamuzu wa Mahaka Kuu

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

Jopo la mawakili nane nguli wa Serikali wamewasilisha hoja kumi katika Mahakama ya Rufaa wakipinga maamuzi ya Mahakama Kuu kuruhusu mashtaka yasiyo na dhamana yawe na dhamana na kubainisha kuwa kifungu kinachozuia kinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mawakili hao wanamwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali hoja zao zilisikilizwa mbele ya jopo la majaji watano akiwemo Jaji Stella Mugasha, Dk. Gerald Ndika, Jacob Mwambegele, Mwanaisha  Kwariko na Ignas Kitusi.

Jopo la mawakili hao ni Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, Mawakili Wakuu wa Serikali, Alesia Mbuya, Faraja Nchimbi, Tumaini Kweka, Abubakar Mrisha na Narindwa Sekimanga waliwasilisha hoja wakiomba mahakama hiyo ya juu itengue maamuzi ya Mahakama Kuu.

Miongoni mwa hoja walizowasilisha ni kwamba Mahakama Kuu ilikosea  kisheria kutamka kuwa kifungu namba 148(5) kinakiuka Ibara ya 13(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Mahakama hiyo ilifanya makosa ya kisheria kutamka kuwa Kifungu hicho namba 148 cha sheria ya makosa ya jinai hakithibitishwi na Ibara ya 15(1) na (2)(a ) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Warufani wanadai mahakama hiyo ilikosea kutamka kwamba kifungu hicho kilikiuka Katiba pamoja na kwamba mjibu rufaa alishindwa kuthibitisha madai yake bila kuacha shaka.

Jopo la mawakili hao linadai Mahakama ilikosea kuamua kwamba Katiba ilikiukwa kwa kuangalia hoja zisizosanifiwa , ilikosea kupinga kifungu hicho bila kuzingatia shida zinazoweza kusababishwa katika mfumo mzima wa utawala wa haki za Jinai nchini

Warufani pamoja na mambo mengine wanaomba mahakama hiyo itengue Hukumu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles