|Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali imesema mabadiliko yanayotokea katika uchaguzi mdogo wa ubunge, hayaathiri idadi ya viti maalumu vya chama husika.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Maunde amesema hayo akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Angelina Malembeka aliyetaka kujua hatima ya wabunge walioingia bungeni kupitia asilia za majimbo yao ya uchaguzi.
“Kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeongeza idadi ya majimbo, je ni lini wabunge wapya wa CCM kupitia viti maalumu wataingia bungeni?” alihoji Malembeka.
Akijibu swali hilo Mavunde amesema idadi ya wabunge wa Viti Maalumu kwa kila chama inapatikana wakati wa uchaguzi mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.
“Hata hivyo, serikali imeendelea kupokea maoni na ushauri kuhusu jambo hili, kutokana na hali ilivyo kwa sasa Katiba na Sheria za nchi vitaendelea kuwa msingi mkuu wa ufafanuzi na mgawanyo wa wabunge wa viti maalumu bungeni,” amesema Mavunde.