29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MAUZO YA SILAHA YAONGEZEKA MASHARIKI YA KATI

STOCKHOLM, SWEDEN


MAUZO ya silaha katika nchi zinazokabiliwa na migogoro Mashariki ya Kati, yameongezeka mara mbili katika kipindi cha miaka mitano iliyopita huku Marekani na Ulaya zikisafirisha shehena kubwa ya silaha.

Kwa mujibu wa  taasisi  ya kimataifa ya Stockholmm, inayohusika na masuala ya amani (SIPRI) – mauzo ya silaha katika mataifa ya Mashariki ya Kati yaliongezeka kwa asilimia 103 kipindi cha miaka 2013-2017 kulinganisha na miaka mitano iliyopita.

Mtafiti  wa SIPRI, Pieter Wezeman katika taarifa yake alisema kuongezeka kwa migogoro katika Mashariki ya Kati na wasiwasi kuhusu haki za binadamu kumesababisha kuwepo mijadala ya kisiasa Ulaya Magharibi  na Amerika ya Kaskazni, juu ya haja ya kuzuia mauzo ya silaha.

Hata hivyo, Marekani na nchi za Ulaya zinabakia  kuwa wauzaji wakuu wa silaha, zikisafirisha zaidi ya asilimia 98 ya silaha zilizoingizwa nchini Saudi Arabia.

Saudi Arabia inayoongoza kampeni kubwa ya kijeshi dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen, imeshuhudia ununuzi wake wa silaha ukiongezeka kwa asilimia 225 katika kipindi hicho kulinganisha kilichotangulia cha miaka 2008-2012.

Utafiti huo wa SIPRI umezidi kubainisha kuwa Marekani ilidhihirisha kuwa ndio nchi inayoongoza duniani  kwa kuuza silaha nyingi zaidi kipindi hicho, baada ya kuuza karibu theluthi moja ya silaha huku katika mataifa ya Mashariki ya Kati yakiwa nusu ya silaha zote zilizouzwa.

Kwa mujibu wa ripoti, kutokana na mikataba ya mauzo ya silaha iliyosainiwa huko nyuma, Marekani itaendelea kuwa taifa linaloongoza kwa kuuza silaha nyingi zaidi duniani katika miaka ijayo.

Urusi, Ufaransa, Ujerumani na China zimeungana na Marekani na kuwa nchi kubwa zinazoongoza kwa mauzo ya silaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles