28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

NKURUNZIZA ATANGAZWA KIONGOZI WA MAISHA CHAMA TAWALA

BNUNJUMBURA, BURUNDI


CHAMA tawala nchini Burundi (CNDD/FDD), kimemtangaza Rais Pierre Nkurunziza kuwa kiongozi mkuu wa kudumu wa chama hicho.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa (CNDD/FDD) uliofanyika Buye, Kaskazini mwa Burundi mahali alikozaliwa Nkurunziza.

Hayo yamejili wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya Katiba ili kumruhusu Rais Nkurunziza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Taaarifa fupi ya CNDD/FDD iliyotolewa jana ilieleza kuwa vikao hivyo vilinuia kuimarisha chama tawala na taasisi zake.

Sambamba na hilo, chama hicho kimepitisha uamuzi wa kumuongezea hadhi Rais Nkurunziza kwa kumpa cheo cha juu. Kimemtangaza kuwa kiongozi mkuu wa kudumu ndani ya chama.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CNDD/FDD, Evariste Ndayishimiye aliutangazia umati wa wananchi waliokuwa katika hafla ya makundi ya utamaduni ya chama tawala azimio hilo, alilosema ni muhimu  katika uhai wa chama tawala.

Tangazo kumfanya Rais Nkurunziza kuwa Kiongozi Mkuu wa Kudumu wa CNDD/FDD linajiri wakati Burundi inajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu marekebisho ya Katiba inayotarajiwa kupigwa Mei, mwaka huu.

Ikipitishwa itamuwezesha Rais Nkurunziza kuwania urais mpaka mwaka 2034.

Wadadisi wa siasa za Burundi wanaamini hatua hiyo ya chama tawala inanuwia kumaliza mapema mjadala wa mtetezi wa kiti cha urais kwa niaba ya chama hicho na kuonyesha mustakabali wa uongozi kabla hata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

Lakini pia uamuzi huo unapeleka ujumbe kwa wafuasi wa CNDD/FDD na haswa viongozi wenye nia pengine ya kuwania nafasi hiyo na hivyo kujaribu kukiepusha chama tawala na mpasuko kama ilivyotokea mwaka wa 2015 katika mzozo kuhusu muhula wa sasa wa Rais Nkurunziza.

Isitoshe kwa wachambuzi wa siasa wanaiona hatua hii kuwa dalili tosha ya jinsi kiongozi huyo alivyokidhibiti chama hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles