25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mauzo ya Pamba, Choroko yaingiza Bilioni 1.3

Na Allan Vicent, Tabora

Wakulima wa zao la pamba na choroko wilayani Igunga mkoani Tabora wamepata mafanikio makubwa katika kilimo cha mazao hayo kwa msimu wa 2020/2021 baada ya kufanikiwa kuuza zaidi ya kilo 250 za pamba na kilo 700,000 za choroko na kupata zaidi ya sh bil 1.3.

Hayo yamebainishwa juzi na Kaimu Meneja Mkuu wa Chama Cha Ushirika wa Wakulima wa Pamba Mkoani hapa (Igembensabo), Juma Mrisho alipokuwa akiongea na Mtanzania Digital ofisini kwake.

Amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi kubwa zilizofanywa na serikali kwa kuwaletea mbolea kwa wakati ikiwemo utoaji elimu ya kilimo bora na hamasa iliyotolewa na Balozi wa zao la pamba nchin, Aggrey Mwanri.

Aliongeza kuwa uamuzi wa serikali kuifanya wilaya hiyo kuwa eneo la kimkakati na kitovu cha uzalishaji wa mbegu bora za pamba kwa ajili ya kuwasambazia wakulima katika mikoa yote nchini umeongeza ari na kasi ya kilimo cha zao na mazao mengineyo.

‘Katika msimu uliopita wakulima walifanya vizuri sana katika kilimo cha pamba na choroko, uzalishaji uliongezeka mara 2, na walipata bei nzuri hivyo wakauza pamba na choroko yote waliyovuna’, alisema.

Mzee Olingo Sombe (68) Mwalimu Mstaafu na mkulima ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha msingi Igunga Balimi Amcos alisema katika msimu uliopita wamepata manufaa makubwa kutokana na usimamizi mzuri wa zao hilo.

“Tulizalisha zaidi ya kilo 250 za pamba na kilo laki 7 za choroko na tumeuza zote kwa fedha taslimu hakuna kampuni hata 1 iliyolaza deni la wakulima, tunaishukuru serikali kwa kusimamia vizuri sekta ya kilimo,” amesema.

Ameongeza kuwa kutokana na mafanikio hayo matarajio yao katika msimu huu ni kuzalisha zaidi ya kilo 1000 ili kuongeza mapato yao, alishauri serikali kuingilia kati suala la bei za pembejeo kwa kipindi hiki ili lisikwamishe jitihada zao.

Naye Katibu Meneja wa Chama cha Msingi, Balimi Amcos, Adelina Boazi amesema mwaka jana walipata mafanikio makubwa kutokana na bei nzuri ya soko na wanunuzi wasio na ubabaishaji hivyo akashauri wakulima kuandaa mashamba mapema na kuzingatia kanuni za kilimo bora ili kuongeza uzalishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles