24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mauzo Soko la Hisa yashuka

patrick-mususaJOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

IDADI ya mauzo ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), wiki hii imepungua kwa asilimia 23 hadi kufikia Sh bilioni 6.4 kutoka Sh 8.3 bilioni wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Meneja wa Mauzo wa DSE, Patrick Mususa, alisema licha ya mauzo kushuka, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeongezeka mara sita  hadi milioni 11 kutoka milioni 1.8 wiki iliyopita.

Alisema Benki ya CRDB imeongoza kwa kuwa na wingi wa hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa asilimia 95.45 zikifuatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL Group) kwa asilimia 2.18 na DSE kwa asilimia 1.44.

“Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa wastani wa asilimia 2.1 hadi Sh. trilioni 21.4 kutoka Sh trilioni 21.9 na ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia umepungua kwa wastani wa asilimia 0.3 hadi trilioni 8.19 kutoka trilioni 8.21 wiki iliyopita.

“Kwa upande wa viashiria, sekta ya viwanda imepungua kwa wastani wa pointi 17.7, baada ya bei ya hisa za TCC kupungua kwa asilimia 1.7
na sekta ya huduma za kibenki na kifedha wiki hii imepungua pointi 4.5, baada ya bei ya hisa za DSE kushuka kwa asilimia 6,” alisema Mususa.

Alisema kiashiria cha sekta ya huduma za biashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 3,157 sawa na wiki iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles