28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

MAUAJI YA WATOTO YAZIDI KUTIKISA NJOMBE

Na Elizabeth Kilindi

-Njombe

SIKU mbili baada ya Kikosi Maalumu cha Operesheni kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini kutua mkoani Njombe chini ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani, kwa ajili ya kuchunguza matukio ya mauaji ya watoto, mtoto  mwingine wa saba amechinjwa na watu wasiojulikana.

Mtoto huyo wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Matembwe, Tarafa ya Lupembe, ametajwa kwa majina ya Rachel Malekela (7), alichinjwa juzi jioni na mwili wake kukutwa kwenye kichaka mita 120 kutoka mahali ilipo nyumba yao.

Katika mwendelezo wa matukio hayo, watu watatu wameuawa na wananchi wenye hasira na mwingine mmoja amejeruhiwa wakihusishwa na matukio hayo ya utekaji na mauaji ya watoto wilaya za Wanging’ombe na Ludewa.

Juzi baada ya kutua Njombe, Kamishna Marijani, alisema yeye si mtu wa maneno mengi akiahidi kupata taarifa za watu wanaotekeleza unyama huo kwa shari au kwa hiyari.

MTOTO ALIVYOUAWA

Wakizungumzia tukio la kuuawa kwa mtoto huyo, wakazi wa Kata ya Matembwe walisema alitoka shule na kufika nyumbani na baadaye kumfuata mama yake aliyekuwa shambani akipalilia ambako si mbali na nyumbani.

“Ni kawaida yake huyu mtoto anapotoka shule kumfuata mama yake shambani, alichezacheza halafu akamwambia mama  yake anarudi nyumbani na hivyo kumpa maagizo ya kazi za kufanya na alipofika hakufanya bali alikwenda ….

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles