24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mauaji ya kinyama yarejea Geita

NA VICTOR BARIETY, GEITA

MAUAJI ya kinyama ambayo yanahusishwa na imani za kishirikina yameanza kurejea mkoani Geita, baada ya watu wanne wa familia moja wakazi wa kijiji cha Bugalama wilayani Geita kuuawa.

Watu ambao majina yao hajatambuliwa mara moja, wameuawa kwa kuchinjwa shingo kama kuku.

Waliouawa katika tukio hilo lililotokea Desemba Mosi, ni wanawake watatu na mtoto mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Latson Mponjoli alipoulizwa jana alikiri  kutokea kwa tukio hilo.

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Mponjoli alisema hivi karibuni mkazi wa kijiji hicho, Samweli Masibo alifariki dunia,baada ya kuugua maradhi ya kawaida.

Alisema marehemu Masibo alikuwa na wake watatu na siku chache baada ya kufariki dunia alianza kuonekana kwa njia za kishirikina nyumbani kwa mke wa pili ambaye kwa sasa ni marehemu.

“Wanasema eti marehemu alikuwa anaonekana usiku nyumbani kwa mke wa pili na kwamba hakufariki,  bali aliuawa kishirikina masuala ambayo sisi hatuwezi kuyathibitisha’’alisema Kamanda Mponjoli.

Alisema  jana (juzi) wakati familia hiyo ikiwa inaota moto  usiku lilitokea kundi la watu ambao hawakujulikana mara moja, wakiwa na silaha za jadi na kuanza kushambulia kila mtu aliyekuwa mbele yao na kusababisha vifo  hivyo.

‘’Kwa kweli hili tukio linasikitisha,wameuawa kinyama wametenganishwa vichwa na kiwiliwili…polisi tumeanza kuchukua hatua.Tunaomba mtuvumilie kesho (leo) tutawapa majina yote ya marehemu,’’alisema mponjoli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles