26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mauaji ya Khashoggi yalitokea chini ya uangalizi wangu-Mwanamfalme

SAUDI ARABIA

MWANA wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman amesema anakubali kuwajibika na mauaji ya mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi yaliyotekelezwa na mawakala wa nchini humo mwaka jana.

Kwa mujibu wa makala  ya shirika la PBS ambayo inatarajiwa kuchapishwa, Salman amesema anakubali kuwajibika katika mauaji hayo kwa sababu  yalitokea chini ya uangalizi wake.

Salman hajawahi kuzungumza hadharani juu ya mauaji hayo yaliyotokea ndani ya ubalozi wa Saudia Arabia mjini Istanbul.

Shirika la Kijasusi la Marekani la CIA na baadhi ya nchi za Magharibi zilimshutumu kwamba yeye ndiye aliyetaka yatekelezwe, lakini maofisa wa Saudi Arabia walisema yeye hana jukumu hilo.

Kifo hicho kilizua ghadhabu duniani kote, na kuchafua taswira ya mwana wa mfalme huyo  na kuiweka nchi hiyo ambayo ni msafirishaji mkubwa wa mafuta katika mipango ya hatari ya uchumi.

Tangu wakati huo hajawahi kutembelea Marekani au Ulaya.

“Yalitokea chini ya uangalizi wangu. Nawajibika kwa yote,” alimwambia  Martin Smith wa PBS.

Kwa mujibu wa tangazo la makala hiyo iliyomuhoji mwana wa mfalme huyo imepangwa kurushwa hewani Oktoba 1, mwaka huu wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kitokee kifo cha Kashoghi.

Ripoti ya Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ilieleza kuwapo kwa ushahidi kamili kwamba mwanamfalme huyo wa Saudia Salman na maafisa wengine wa ngazi za juu wanahusika kibinafsi kwa muaji ya Khashoggi.

Ripoti ya mtaalamu huyo wa UN Agnes Callamard ilisema kuwa ushahidi huo unahitaji kufanyiwa uchunguzi na jopo huru la kimataifa lisilipoendelea upande wowote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles