25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyakazi CRDB mbaroni kumuibia mteja zaidi ya milioni 100

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo, Andrew Babu (27) na wafanyabiashara watatu, wameshtakiwa kwa kula njama, kughushi Tembo kadi ya mteja, wizi wa zaidi ya Sh milioni 100 na kutakatisha fedha hizo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, William Sige (52), Justina Boniphace (49) na Alli Tutupa (35) wote wanaishi jijini Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo  Simon akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mbando alidai kati ya Oktoba 2018 na Aprili 19, 2019 washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama  kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka jingine imedaiwa, Oktoba 29, mwaka jana katika benki ya CRDB tawi la Ubungo, ndani ya manispaa ya Ubungo, mshtakiwa Babu peke yake kwa nia ya kulaghai au kudanganya, alighushi sahihi ya Charles Kihamia katika fomu ya maombi ya Tembo card.

Pia mshtakiwa Babu anadaiwa, Novemba 6, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu anadaiwa Novemba 5, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika usajili wa kadi ya visa ya Tembo, kwa madhumuni ya kuonesha kuwa sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Inadaiwa Novemba 6,2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili wa uelekezaji  kwenye fomu ya maombi kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli. 

Mshtakiwa Babu pia anadaiwa, Oktoba 29, 2018 huko katika benki ya CRDB, alitoa  fomu ya kughushi ya maombi ya Tembo kadi  kwa ofisa wa banki hiyo aitwaye Omary Mduyah  kwa dhumuni la kuonesha kuwa fomu hiyo imetolewa na kusainiwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la mwisho, imedaiwa kati ya Novemba 7,2018 na Aprili 29,2019  washtakiwa hao kupitia kadi ya gold ya Visa, walijipatia sh. 106,267,907/-  kutoka kwa Charles Kihamia kupitia Visa gold card huku wakijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kughushi na wizi.

Hata hivyo wa washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles