26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mathayo ahimiza wananchi kujitokeza kuhesabiwa

Na Shomari Binda, Musoma

MBUNGE wa Musoma Mjini, Vedastus Mathayo amewahimiza wananchi jimboni humo kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 23, mwaka huu.

Akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa uhamasishaji uliofanyika Agosti 4, 2022 katika soko la Saa Nane, Mathayo amesema zoezi hilo ni muhimu na kila mwananchi anapaswa kushiriki.

Amesema anapokuwa bungeni kuwakilisha wananchi na kuomba masuala mbalimbali ni muhimu kujua idadi ya wale unao waombea.

Mathayo amesema mji wa Musoma umekuwa na ongezeko la watu kutoka maeneo mbalimbali hivyo Sensa ya Agosti 23, itaisaidia Serikali kupanga mipango yake.

Amesema katika huduma za afya serikali ikitambua idadi ya watu waliopo jimbo la Musoma mjini italeta hudma zinazotosheleza ikiwamo dawa zinazo tosheleza.

“Zoezi hili ni muhimu na serikali ina malengo mazuri katika kuwafikishia huduma wananchi, tusije tukapotoshwa na mimi nitazunguka kila kata kuhimiza wananchi kila mmoja kuhesabiwa ifikapo Agosti 23,” amesema Mathayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Wilaya ya Musoma ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo amesema wamejipanga kufika kila eneo kutoa elimu ya sensa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles