Matatani kwa kutoa rushwa ya 200,000 aandikiwe hana corona

0
657

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imemkamata Mtaalamu wa nyama, raia wa Kenya Alexander Mwikali (42) ambaye anaishi Nkuhungu jijini hapa kwa kosa la kutoa rushwa ya Sh 200,000 kwa Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi  kama kishawishi ili apatiwe cheti cha uthibitisho wa kutokuwa na ugonjwa wa corona.

Aidha, Mkuu huyo wa Takukuru amesema Jumatatu, Takukuru kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itamfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, aliyekuwa Mhasibu Msaidizi Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Severo Mutegeki (42).

Kibwengo amesema Mutegeki atafunguliwa shauri la uhujumu uchumi ambapo atashtakiwa kwa makosa matatu ya matumizi mabaya ya Mamlaka, ubadhilifu na kuisababishia Mamlaka hasara ya zaidi ya Sh milioni 428 kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200, marejeo ya mwaka 2019.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here