30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Ndugulile aipongeza TTCL, aitaka kuacha kufanyabiashara kwa mazoea

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujiendesha kwa faida na kupunguza hasara kwa kipindi cha miaka mitano.

Dk. Ndugulile ameyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha utendaji kazi wa Mameneja wa Mikoa yote wa Tanzania Bara na Zanzibar wa TTCL na Menejimenti ya Shirika hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi la Zimamoto, Dodoma.

“Mmefanyakazi nzuri sana mimi niwapongeze, kutoka kujiendesha kwa hasara mpaka kuja kwenye faida hili ni jambo la kupongezwa kwa TTCL, niwatake sasa muongeze nguvu na kuacha kufabiashara kwa mazoea.

“Hivyo ongezeni ubunifu ikiwamo kufanya utafiti wa masoko ili kubaini mahitaji ya wateja, kuongeza wateja na kwenda sambamba na ushindani kwa kuwa mpaka sasa TTCL ina asilimia mbili ya wateja wa simu za mkononi kwenye soko ukilinganisha na kampuni nyingine na jumla ya wateja milioni 1.3 wa simu za mkononi,” amesema Dk. Ndugulile.

Aidha, katika kikao hicho, Dk. Ndugulile amewaita Mameneja wa Mikoa yote ya TTCL nchi nzima ili wajadaliane na kuweka malengo yanayopimika kwa kuwa hivi sasa kiasi cha Sh trilioni 12 zinazunguka kwenye huduma ya fedha mtandao kwa mwezi na miamala isiyozidi milioni 300 kwa mwezi zinapita mtandaoni ili TTCL itumie fursa hiyo kufanya biashara na kutoa gawio.

“Kila Meneja wa Mkoa wa TTCL apewe malengo ya kuongeza wateja, kushughulikia malalamiko ya wateja kwa wakati, kutoa huduma nzuri kwa wateja na kuhakikisha kuwa ukuaji wa kuridhisha wa TTCL unaonekana,” amesema Dk. Ndugulile.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alimemweleza Dk. Ndugulile kuwa Shirika lake limeweza kujiendesha kwa faida kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2016/2017 kwa kutengeneza faida ya Sh bilioni tano kwa mwaka tofauti na miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2016 kurudi nyuma ambapo Shirika limekuwa likijiendesha kwa hasara.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Jim Yonazi amewaeleza Mameneja hao kuwa watumie mbinu za kuongeza wateja na kutengeneza mazingira ya kukubalika katika maeneo wanayotoa huduma kama ilivyo kwa waganga wa tiba za asili na wahubiri wa dini ambapo wamejenga imani na wanatoa huduma kwa wafuasi wao

Pamoja na kikao hicho, washiriki wamepatiwa mada kuhusu Mkakati wa kurahisisha Uongozi na Ushirikiano na Ofisi za Serikali Mikoani na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka kwa Johnson Nyingi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na mada kuhusu utawala bora kutoka kwa ,Apolinari Tamayamali, Mkurugenzi wa Utawala Bora, Ofisi ya Rais – Ikulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles