25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mataifa 75 kushiriki maonesho ya elimu UAE

Mohamed Al Bulooki
Mohamed Al Bulooki

ABU DHABI, UAE

MUUNGANO wa Falme za Kiarabu (UAE) unaandaa maonesho ya kimataifa ya elimu ya ufundi stadi na ujuzi yatakayoshirikisha mataifa 75.

Maonesho hayo yanayojulikana kama ‘Worldskills Abu Dhabi 2017’ yatakayodhaminiwa na Shirika la Ndege la Etihad, yatakutanisha washiriki na wataalamu zaidi ya 3,000 kuanzia Oktoba 14 hadi 17, 2017.

Yakiwa maonesho ya 44, yatafanyika mara ya kwanza katika ukanda wa Mashariki ya Kati ikiwa ni tukio kubwa litakaloratibiwa na Kampuni ya Maonesho ya Taifa Abu Dhabi (ADNEC).

Maonesho hayo ya Worldskills Abu Dhabi 2017 yanalenga kuongeza hadhi kwa wanafunzi wanaosomea elimu ya ufundi ili wawe bora zaidi na wenye ufanisi katika kile walichosomea.

Makamu wa Rais wa Etihad, Mohamed Al Bulooki, alisema: “Ni heshima kubwa kwetu kutambulika kama mdhamini rasmi wa mashindano hayo makubwa duniani.

“Mji wa Abu Dhab ni wa kisasa na umekuwa kitovu cha biashara na utalii duniani. Washiriki watapata fursa ya kujifunza mambo mazuri ikiwamo ukarimu kwa wenyeji na kushuhudia miundombinu mizuri ya mji huu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles