32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MASWALI MAGUMU WAKATI WA USAHILI OXFORD

Na Joseph Lino


CHUO Kikuu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza ni chuo chenye sifa na heshima katika utoaji wa elimu ya taaluma mbalimbali duniani.

Chuo cha Oxford ambacho kilianzishwa miaka ya 1096 hadi sasa kinaendelea kuwa chuo bora ulimwenguni.

Chuo hicho hutumia mfumo wa usahili katika kuchagua wanafunzi ambao wanataka kujiunga chuoni hapo.

Inafahamika duniani kote kuwa wanafunzi wanaojiunga katika ngazi mbalimbali Oxford huwa na sifa au vipaji maalumu.

Walimu wanaofundisha chuoni hapo huwapima mwanafunzi kwa uwezo wake wa kufikiri, maarifa na kuweza kutatatua changamoto kwa njia mbalimbali.     

Kila mwanafunzi anayedahiliwa Oxford lazima ajielewe vizuri kwa sababu hawahitaji mtu ambaye ana uwezo wa kukariri.

Mwanafunzi kabla haujadahiliwa kwenye chuo hicho hufanyiwa usahili kupima uwezo wake wa kufikiri.

Usahili huo si tu wa kukariri kichwani kitu ambacho unakijua, lakini usahili huo unatungwa kwa lengo la kumpa mwanafunzi nafasi ya kuonyesha uwezo na nguvu ambayo inahamasisha kutumia maarifa katika kutatua matatizo mapya.

Pia maarifa hayo yanamwezesha mwanafunzi kuwa mbunifu katika nyanja mbalimbali kwa namna mbili ambayo inamletea changamoto au kumruhusu kuwa bora.

Mkurungezi wa wanafunzi wa Shahada wa Oxford, Samina Khan anasema wakati wa kujibu maswali hayo si kitu ambacho unajua kipo sahihi, lakini kukabiliana na mawazo mapya.

Hata hivyo, maswali ya usahili huo huwa changamoto kwa wanafunzi wengi kwa sababu yanahitaji maelezo binafsi, mara nyingi watu huyaona maswali hayo ni ya kijinga lakini yanakuwa na tija ndani yake.

Asilimia kubwa ya wanafunzi hushangaa namna ya maswali huulizwa au kuletwa katika mtihani.

Wanafunzi wanajikuta wakifeli katika usahili wa kujiunga na masomo ya juu ya Oxford.  

Mwanafunzi mmoja aliwahi kusema kuwa walimu wa oxford wao wanatafuta mtu ambaye ana akili za kawaida (natural intelligent) na mwanafunzi ambaye mwalimu atakuwa na furaha kumfundisha.

Haya ni baadhi ya maswali ambayo huulizwa katika usahili wa kudahiliwa chuo cha Oxford.

 

1.       Kinachotofautisha hadithi fupi na riwaya ni nini?

  1. Fikiria hatukuwa na rekodi ya kumbukumbu ya historia ya kipindi cha nyuma, isipokuwa kuna rekodi za kukumbuku ya kila kitu kinachohusiana na michezo. Ni kiasi gani cha kumbukumbu tunaweza kupata kuhusiana na michezo?
  2. Kwanini binadamu huwa ana macho mawili?
  3. Je, ni lazima mashairi yawe magumu kueleweka?
  4. Je, vurugu zinazotokea huwa ni za kisiasa? Je, siasa inamaanisha kitu tofauti katika mazingira tofauti?
  5.  Kama kuegesha gari katika mistari miwili ya njano adhabu yake ni kifo, na hakuna aliyewahi kutenda kosa hilo je, hiyo inaweza kuwa sheria mahususi?
  6.  Ni kitu gani cha kawaida kwa binadamu?
  7. Kama unaweza kugundua chombo kipya cha muziki, ni aina gani ya sauti kitakuwa kinatoa?
  8. Huu ni mti wa cactus. Niambie kuhusu huu mti.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles