27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Master Jay: Wana hip hop hawajui kutumia fursa  

DSC_7394NA FESTO POLEA

 PRODYUZA maarufu nchini, Joachim Kimaryo “Master Jay’, ameweka wazi kwamba licha ya muziki wa hip hop kupendwa zaidi lakini wasanii wake hawajui kuutumia muziki huo kimafanikio.

Master Jay aliliambia Mtanzania kwamba licha ya wana hip hop wa Tanzania kuwa na uwezo mkubwa katika kazi zao za muziki, hawajui namna ya kutumia fursa zinazowazunguka kama wafanyavyo wasanii wa Kimarekani.

Alisema wana hip hop wa Marekani waliokuwa wajanja walipata jina kwenye hip hop lakini fedha wakapata kupitia vifaa vyao akiwemo Jay Z, P didy, 50 Cent na wengine wengi.

“Wana hip hop wa Kimarekani wengi wametumia muziki huo kutengeneza jina na jina lao ndilo lililotengeneza mafanikio yao tofauti na wana hip hop wa hapa Bongo, wanasubiri muziki uwalipe badala ya kuangalia na fursa nyingine kama wanavyofanya Wamarekani,” alieleza.

Master Jay aliongeza kwa kuwataka wana hip hop nchini kujifunza kupitia wasanii hao wa Marekani namna wanavyotumia fursa kujiingizia kipato badala ya kung’ang’ania muziki ili uwafikishe wanakotaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles