28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mastaa walivyoweka ustaa pembeni kwenye harusi ya Shamsa Ford

IMG_3728

NA KYALAA SEHEYE,

INAWEZEKANA huu mwaka ukawa ni mwaka uliovunja rekodi kwa mastaa wengi kuingia kwenye mapenzi ya ndoa. Haina shaka kwa sababu inaonekana wazi wasanii wa kiume wameamua kuoa na wasanii wakike nao wameamua kuolewa.

Nyota mbalimbali kutoka kwenye tasnia ya muziki na filamu kama vile Roma, Baghdady, Manecky, Ricardo Momo, Menina, Mr Blue, Masanja Makandamizaji wote hao wameamua kuachana na ukapela na kuingia kwenye ndoa jambo lililoleta picha nzuri kwa jamii inayowatazama kama kioo.

Orodha hiyo ya wasanii walioingia kwenye ndoa imeongezeka siku ya Ijumaa wiki iliyopita kwa Diva kutoka kiwanda cha filamu nchini, Shamsa Ford, kuolewa na mfanyabiashara maarufu wa mavazi nchini, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’.

Hii ni ndoa iliyofanikiwa kuteka mitandao ya kijamii na habari yake imekuwa kubwa kiasi kwamba hivi sasa hakuna ambaye hafahamu kubwa Shamsa ni mke halali wa Chid Mapenzi.

Ndoa hiyo ilifanyika nyumbani kwa kina Shamsa Ford maeneo ya Sinza Africa Sana na ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wasanii, wanahabari, ndugu na jamaa kutoka pande zote mbili.

Kwa kuwa kwenye matukio makubwa kama haya, watu maarufu huwa wanatazamwa zaidi basi acha Juma3tata, ikusogezee nyota mbalimbali waliohudhulia kwenye harusi ya Shamsa Ford na matukio ambao waliyafanya muda wote wa tukio hilo adimu kutokea kwenye tasnia ya filamu.

Juma3tata ilizinasa sura za mastaa hawa wa kiume Haji Adam, Dully Sykes, P the Mc, Niva, Jimmy Mafufu, Duma, Richie Richie, Rado, Willium Mtitu, Steve Nyerere na wengine wengi huku Jb akipata tatizo la kiafya na kulazimika kuondolewa eneo la tukio kabla hajashuhudia utamu wa tukio hili la kuolewa kwa binti aliyegundua kipaji chake.

Kumekuwa na mtazamo hasi kwenye jamii kuwa wasanii hasa wakike hawapendani. Kama na wewe ulikuwa unafikiria hivyo naomba nikwambie kuwa haupo sahihi na unakosea, kupitia harusi ya Shamsa, tumefahamu kuwa kuna umoja unaoitwa Wanawake wa Tasnia

Ndani ya umoja huu unakutana na warembo wengi wanaounda tasnia ya filamu nchini kama vile Blandina Chagula ‘Johari’, Aunty Ezekiel, Grace Mapunda, Thea, Halima Kimwana, Ester Kiama, Jacline Wolper, Riyama Ally na wengine wengi.

MASTAA WAUVUA USTAA

Ndoa ni jambo la heri hivyo hadhi yako kwenye jamii siyo vyema sana ukiileta kwenye tukio kama lile na hapo ndipo mastaa wakike walipoamua kuuvua ustaa wao na kuamua kujichanganya na watu wengine kucheza vigoma, aina ya muziki unaobamba hivi sasa kwenye mitaa ya uswahilini.

Wakati mastaa kama vile Aunt Ezekiel wakionyeshana ujuzi wa kuzungusha nyonga wakati wa ngoma hizo za uswahili zikipigwa na kikundi kilichoalikwa pale, Mc wa shughuli alizuia kabisa picha na video zisichukuliwe ili kuwa na usiri wa jambo lile lililovuta hisia za watu wengi.

WANAWAKE WA TASNIA WAFUNIKA

Hainaga Ushemeji Tunakula, ni ngoma ya Man Fongo iliyowatoa kwenye viti wasanii wakike wanaounda umoja wa Wanawake wa Tania na kusogea mbele ya wanaharusi kwa ajili ya kutoa zawadi yao kwa mwana umoja mwenzao, Shamsa Ford.

Mwenyekiti wa umoja huo, Ester Kiama ndiyo alianza kutambulisha viongozi akianza na Mama wa nidhamu ambaye ni Aunt Ezekiel, muweka hazina ambaye ni Odama na Joan ndiyo katibu msaidizi.

“Kwa sababu ametoka huku sasa hivi mambo ya kupika pika yatakuwa mengi, tume mnunulia jiko la gesi lenye sahani nne lenye thamani ya shilingi Laki 5, tunampa  na fedha taslimu shilingi Milioni 1 hilo jiko tunafanya mpango lipelekwe moja kwa moja nyumbani kwao Upanga na huo mzigo wa hela atapewa hapa hapa,” alisema Easter Kiama.

AUNT EZEKIEL AFUNGUKA

“Wasanii wakike tunaonekana wahuni sana, tunaonekana hatujatulia, tunaonekana tupo tupo tu, lakini tunaamini wewe utaenda kubadilisha mtazamo huo, mjue Mungu, mpende mmeo na katika yote hayo usitusahau marafiki zako kwa sababu ndiyo ndugu zako na ukumbuke kutoka kwenye shughuli za wenzako,” alisema Aunt Ezekiel Mama wa nidhamu kwenye umoja huo.

IRENE UWOYA ATOA OFA

Mkali huyu wa filamu alichelewa kufika. Hivyo akaona apate nafasi ya kipekee ya kumpongeza msanii mwenzake ambaye anasema ameanza kufahamiana naye muda mrefu uliopita.

“Shamsa ni rafiki yangu wa siku nyingi sana, nakumbuka nilipojifungua mwanangu Krish, Shamsa ndiyo alikuwa msanii wa kwanza kumuona mtoto wangu. Kama alivyosema kiongozi wetu wa Wanawake wa Tasnia na zawadi tuliyompa, mimi binafsi nina zawadi ya peke yangu, zawadi ni ndogo tu ambayo Shamsa na mume wake watalala kwenye hotel ya Ramada Resort Mbezi Beach kwa siku tatu,” alisema Irene Uwoya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles