26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

David Luiz sio chaguo sahihi kwa Antonio Conte

David Luiz
David Luiz

NA ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

UJIO wa David Luiz,  kujiunga na timu ya Chelsea jambo la kwanza kukiri ni  kutokuwapo kwa  madhara ya nyota huyo ndani ya uwanja.

Mbrazil huyo anaweza kusaidia kubadili hali ya hewa katika vyumba vya kubadilisha nguo lakini si kuwa na kitu kipya ndani ya uwanja.

Luiz amerejea  Chelsea ikiwa tayari haina ubavu wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya labda kwa msimu huu kumalizika.

Hata hivyo beki huyo  hakuwa chaguo la kwanza la kocha wa Chelsea, Antonio Conte, lakini amefanikiwa kusajiliwa ndani ya kikosi hicho.

Kiwango chake pia hakina ushawishi  wa kutosha  na ndicho kilichosababisha kutoswa na  uongozi wa Paris Saint Germain kuruhusu beki huyo aondoke.

Baada ya  kuporomoka kiwango, rais wa PSG, Nasser al-Khelaifi, na  Mkuu wa benchi la ufundi la timu hiyo,  Patrick Kluivert walikubali beki huyo kuondoka.

Si jambo la kawaida mchezaji tegemeo na hodari kuruhusiwa kuondoka kirahisi katika klabu kama PSG lakini  suala la Luiz halikuwa lenye kuumiza kichwa kwa viongozi hao kumrusu kuondoka.

Kocha wa  PSG,  Unai Emery aliupokea uamuzi huo bila shaka  kwani katika michezo ya awali kabla ya Ligi Kuu Ufaransa kuanza  kocha huyo alithibitisha Marquinho na Thiago Silva ndio chaguo lake la kwanza si Luiz.

Inawezekana uamuzi wa kocha huyo  ulikuwa wa kucheza na akili ya Luiz  kutokana na kiwango alichokionekana katika mchezo wa mwisho ulioshuhudiwa kwa PSG kufungwa mabao 3-1.

Mchezo huo ndio  ulidhihirisha kwamba  Luiz hakuwa na kiwango imara cha kumshawishi kocha huyo kumpanga katika kikosi chake cha kwanza katika msimu mpya wa Ligi kuu ya Ufaransa.

Kutokana na uamuzi huo ndio maana PSG hawakuweka kauzibe sana lilipokuja dili la kuuzwa kwa nyota huyo .

Biashara hiyo ilifanyika siku ya mwisho ya dirisha la usajili kwa Chelsea kutoa  kitita cha pauni milioni 34  ili kupata saini ya nyota huyo.

Hivyo kufanya Luiz kurejea viwanja wa Stamford Bridge tangu mwaka 2014 alipokuwa mchezaji wa timu hiyo.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu aondoke katika klabu hiyo, Luiz anasema kwamba yupo tayari kuvaa jezi za timu hiyo kwa mara ya pili.

Hata hivyo bado beki huyo anadeni la  kulipa kwa mashabiki wa Chelsea kwani wanamwona kuwa ni msaliti baada ya uamuzi wake wa kuikimbia timu hiyo na  kujiunga na PSG.

Mashabiki hao wanaweza kumsamehe licha ya kuwaadhibu  katika michezo ya Ligi ya Mabingwa akiwa PSG.

Lakini kwa upande mwingine Conte anatakiwa kuamini kwamba hajanunua mzigo hivyo lazima atatafuta namna ya kumtumia beki huyo ingawa kwa uharisia biashara ya Luiz haikuwa ya lazima kwa Chelsea.

Kwa sasa Chelsea itakuwa na wakongwe watatu ambao ni walinzi hivyo itampa nafasi nzuri kwa Conte kufanya chaguo  la mchezaji yupi anatakiwa kumtumia katika michezo mbalimbali kama ambavyo aliwahi kufanya akiwa Juventus nchini Italia.

Conte anachotakiwa kufahamu ni kwamba Luiz hana kipya cha kumthibitisha kiwango chake kwa kuwa ameshamaliza kila kitu  PSG  na huenda mwisho wa siku akaondoka  kama mchezaji huru katika klabu hiyo.

Na inavyoonekana  Conte hana mpango na ahadi uchwara za Luiz badala yake anaonekana kuwa makini na  katika kuimarisha ulinzi kwa kumtumia  N’Golo Kanté ambaye anaonekana kuwa muhimili mkubwa wa kikosi chake.

Hamasa aliyonayo Conte kwa Kante ni kubwa mno ambapo kwa sasa amekuwa aambiliki kumtengeneza nyota huyo.

Wakala wa mchezaji  wa Luiz, Kia Joorabchian na  Giuliano Bertolucci  wamekuwa karibu sana na  mmiliki wa klabu ya Chelsea,  Roman Abramovic kwa kipindi kirefu sana.

Kwani ndio waliohusika katika biashara kichaa ya mkopo kwa Alexandre Pato kwa kujiunga na  klabu hiyo.

Tayari Chelsea wana wachezaji kama  John Terry  kwa mkataba wa mwaka mmoja, Kurt Zouma amerejea baada ya maumivu ya muda mrefu wakati Andreas Christensen amepelekwa klabu ya Borussia Mönchengladbach kwa mkopo wa miaka miwili. Lakini Conte mchezaji ambaye anamuangalia ni Konte na wala sio Luiz, lakini Luiz amekuja kutokana na bosi wa timu hiyo.

Wachezaji hao waliotolewa kwa mkopo wamekuwa katika kiwango kizuri katika Ligi ya Bundesliga na huenda  wakarejea England msimu ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles