29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mastaa na ‘bodyguards’ ni ulinzi au mbwembwe?

CHRISTOPHER MSEKENA

KATIKA karne ya 19 huko Hispania, tajiri mmoja aliyetambulika kama King Of Leon, alikuwa anakatiza mitaa yenye vurugu, hivyo akamwomba kijana mwenye misuli na mwili wa miraba minne amsaidie kuvuka salama eneo hilo.

Kijana huyo ni Santa Herman Dad ambaye ni mlizi binafsi wa kwanza duniani, aliyeasisi mtindo wa watu mbalimbali hasa maarufu kutumia ‘bodyguards’ katika suala la ulinzi wanapokuwa maeneo yanayowakutanisha na watu wengi.

Katika siku za hivi karibuni mtindo wa mastaa wa Bongo na majuu kutumia walinzi binafsi, umeshika kasi zaidi kiasi cha kuonekana siyo ulinzi tena bali ni mbwembwe za kutaka uwepo wao eneo husika ujulikane haraka.

Siku kadhaa zilizopita hapa Bongo wakali kutoka WCB, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Harmonize walikuwa gumzo baada ya kuonekana wakiwa na walinzi binafsi wengi katika matukio ya msiba wa Ruge Mutahaba na Ephraim Kibonde.

Mastaa hao kwa sasa ndiyo wanaongoza kuwa na walinzi binafsi ambao huambatana nao kila sehemu wanapokwenda ikiwamo kwenye shoo na matukio mengine ya kijamii.

DIAMOND PLATNUMZ
Huyu ndiyo msanii mwenye walinzi binafsi wengi zaidi hapa Bongo, itakumbukwa Machi 2, mwaka huu Diamond Platnumz, alitua katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, kuaga mwili wa Ruge Mutahaba lakini akaishia kuondoa utulivu kwa waombolezaji.

Staa huyo atinga viwanjani hapo kwa kuchelewa, akiwa na walinzi binafsi zaidi ya watano na kusababisha watu kumtazama huku wengine wakimshangaa, jambo lililofanya wana usalama kumzuia kuigia ndani kutoa heshima zake za mwisho kwa Ruge.

“Ili msanii ufanye vizuri kwa sasa unahitaji mambo mengi kama hivi timu kubwa ya mameneja, wapiga picha na huu ulinzi wa ma ‘bodyguard’ ni mkwara tu sababu tunaonekana wasanii wakubwa, watu wasije wakatukaba,” anasema Diamond Platnumz alipokuwa akitoa hoja katika kikao cha wasanii na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Januari 25, 2019.

Wakati Diamond Platnumz anasema hayo, mashabiki wengi wameendelea kuona staa huyo anawatumia walinzi wake binafsi kama mbwembwe ili kila atakapoingia wajue Chibu ameingia kwa kuwa hasimu wake, Ali Kiba ambaye naye ana ushawishi mkubwa kwenye jamii hana mlinzi hata mmoja.

HARMONIZE NAYE ATIA NENO
Naye Harmonize, ambaye amekuwa akionekana kuwa na walinzi binafsi zaidi ya wanne katika kile sehemu anayoonekana ameliambia Swaggaz kuwa: “Mimi ni kijana ambaye nimetoka mtaani pia naiogopa kesho, niko radhi shilingi mbili ninazopata kwenye muziki nigawane na vijana wenzangu ndiyo maana unaona nina mpiga picha, meneja msaidizi na ‘body guards’,

“Mtu ambaye atasema Harmonize hustahili kutembea na ‘body guards’ wengi jambo la kwanza inabidi utambue kuwa huyo ‘bodyguard’ nyuma yake kuna watu zaidi ya 20 wanamtegemea kwa hiyo unataka wasipate riziki?,” anasema Harmonize.

MAJUU IKO VIPI?
Huko majuu hasa Marekani, mastaa nao wamekuwa wakitumia ulinzi binafsi hasa wanapokuwa katika matembezi yao mitaa mbalimbali.
Mwaka jana mwana masumbwi nyota duniani, Floyd Mayweather, alizua gumzo baada ya kuonekana akikatiza mitaa ya Atlanta, akiwa katikati ya walinzi watano wenye miili mkubwa kiasi cha yeye kuonekana kama mtoto mbele yao.

Hali kadharika staa wa Hip hop, Kendrick Lamar, mwezi Julai mwaka jana huko Sydney, Australia, aliibua gumzo mtandaoni baada ya kuonekana akilindwa na mlinzi mwenye mwili mkubwa kama inavyoonekana pichani, jambo lililoibua mjadala kuwa anaongozana na njemba hiyo ili kutia mkwara kwakuwa hahitaji ulinzi mkubwa kiasi hicho.

UKWELI NI UPI?
Mwarabu Mirundi maaarufu kama Mwarabu Fighter ni miongoni mwa vijana jijini Dar es Salaam waliojiajiri kupitia kazi ya ulinzi binafsi na alishaonekana kuwalinda mastaa kadhaa akiwamo Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto, Irene Uwoya, Zamaradi Mketema na wengineo na sasa hivi ana kampuni yake ya ulinzi SM Guards Com.

Akipiga stori ya swaggaz juzi, kuhusu mastaa kuwatumia ‘bodyguards’ kama mbwembwe alisema: “Hapana huwezi kuchukulia kama mbwembwe kwa sababu watu maarufu hasa wasanii mara nyingi wanatuchukua kwa ulinzi, wale wana mashabiki wengi ambao katika kuonyesha mapenzi yao wanaweza kujikuta wamewavamia na hapo kuna mawili, msanii aumie au laa, ndiyo maana wanaamua kuwa na walinzi binafsi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles