29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Kufuru mabilioni pete alizowahi kuvalishwa J Lo

SWAGGAZ RIPOTA

STAA wa singo ya Ain’t Your Mama, Jennifer Lopez ‘J Lo’, amerudi kwa kasi kwenye vichwa vya habari za burudani, baada ya kuweka wazi hatua muhimu ya kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Alex Rodriguez katika moja ya fukwe binafsi huko Marekani hivi karibuni.


J Lo mwenye miaka 49, amekuwa gumzo zaidi kutokana na maisha yake ya mapenzi aliyowahi kuishi miaka ya nyuma hasa mtindo wa kuolewa na kuachika mara tatu pamoja na kuvishwa pete kadhaa za uchumba kadhaa.


Washkaji huko mtandaoni wanahoji J Lo ana tatizo gani kiasi cha kutodumu kwa muda mrefu kwenye mapenzi au shida ipo kwa vidume vinavyomtokea mrembo huyo?
Swaggaz, tunakupa thamani ya pete alizowahi kuvishwa J Lo na wanamume mbalimbali aliowahi kuwa nao katika uhuasiano wa kimapenzi.


ALEX RODRIGUEZ
Huyu ni mchezaji wa zamani wa mchezo wa Baseball huko Marekani na ndiye mmiliki wa penzi la J Lo kwa sasa. Aliwahi kuoa mara moja lakini pia kuhusishwa kutoka kimapenzi na warembo kama Madonna, Demi Moore na Cameroon Diaz.


Alex mwenye miaka 43 ambaye amekuwa na mrembo huyo toka mwaka 2017, hivi karibuni alimvisha pete ya uchumba J Lo yenye madini ya almasi inayokadiliwa kuwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 1.4 sawa na shilingi bilioni 3.2 za Tanzania.


CRIS JUDD
2001, J Lo alivishwa tena pete aina ya Emerald yenye thamani ya shilingi 5,956,708 na mwigizaji na dansa maarufu nchini Marekani, Cris Judd licha ya penzi hilo kuvunjika mwaka 2003.


MARC ANTHONY
Mwanamuziki huyu ndiye aliyedumu kwa muda mrefu zaidi na J Lo, toka mwaka 2004 mpaka 2014 walipoachana na katika ndoa yao walibahatika kupata watoto mapacha, Maximilian na Emme.
Enzi za penzi lao, Marc alimvisha pete ya almasi aina ya ‘carat blue’ ambayo ina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 26.2


BEN AFFLECK
Mwigizaji Ben Affleck alimvisha pete J Lo yenye madini ya almasi rangi ya pinki iliyokuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 2.5 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 5.8 za Tanzania.


OJAN NOA
Mwaka 1997, Ojan alimvisha J Lo pete yenye madini ya almasi iliyokuwa na thamani ya dola za Marekani 100,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 200 licha ya penzi lao kuvunjika mwaka mmoja mbele.


JE J LO ATADUMU NA ALEX?
Mbali na pongezi nyiungi ambayo J Lo amezipata kutoka kwa mastaa wenzake na mashabiki, swali ni kwamba ataweza kufunga ndoa na kudumu na Alex Rodriguez?


Hili ni swlai ambalo wawili hao wanaweza kuwa na majibu zaidi kwa kuwa mipango yao wanaifahamu wenyewe licha ya historia zao za kuingia na kutoka kwenye mapenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles